loader
Dstv Habarileo  Mobile
Wanafunzi 2,800 kambi za   wakimbizi wamaliza elimu ya msingi

Wanafunzi 2,800 kambi za  wakimbizi wamaliza elimu ya msingi

WANAFUNZI zaidi ya 2,800 kutoka kambi za wakimbizi wamefanya mitihani ya kumaliza elimu ya msingi.

Wizara ya Usimamizi wa Majanga ilisema mwishoni mwa wiki kuwa, walifanyakazi kwa kushirikiana na Bodi ya Elimu ya Rwanda (REB) na wilaya kadhaa kuhakikisha watoto wa wakimbizi wanafanya  mitihani hiyo kwa usalama.

Ilisema kati ya watahiniwa 254,678 waliosajiliwa kufanya mitihani ya kuhitimu elimu ya msingi, 2868 walitoka kambi sita za wakimbizi zilizoko katika wilaya tofauti.

Ofisa Mawasiliano wa wizara hiyo alisema wanafunzi 92 wa familia zilizohamishiwa katika kambi ya Mahama, wilaya ya Kirehe walifanya mitihani yao kwa kutumia namba za usajili za wilaya ya Gicumbi walikotoka.

Kwa mujibu wa wizara hiyo, wanafunzi wakimbizi 1,702 wamesajiliwa kufanya mitihani ya sekondari inayoanza wiki hii.

Idadi ya wakimbizi wanaoishi Rwanda ni  127,557 hadi mwisho wa mwezi Mei, mwaka huu.

 Wakimbizi hao wanatoka mataifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Burundi na wanaishi katika kambi sita za wakimbizi za   Mahama, Gihembe, Nyabiheke, Mugombwa, Kigeme na Kiziba.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/eda533d35675e461c346306380d62691.jpeg

Katika hali isiyo ya kawaida, Mwanaume mmoja amekutana ...

foto
Mwandishi: KIGALI 

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi