loader
Dstv Habarileo  Mobile
Serikali kusamehe ushuru   wa kuagiza simu za mkononi

Serikali kusamehe ushuru  wa kuagiza simu za mkononi

RAIS Salva Kiir amesema serikali itasamehe ushuru wa kuagiza bidhaa za simu za mkononi ili kuruhusu kampuni kutoa huduma bora kwa raia.

Katika hotuba yake wakati wa uzinduzi wa mtandao wa dijitali juzi, Rais Kiir alisema serikali itasamehe ushuru kwa waagizaji wa vifaa vya mtandao wa simu za mkononi ili kuongeza matumizi ya dijitali  nchini.

"Serikali itafanya maamuzi ikiwa ni pamoja na msamaha wa ushuru ambao utafaidisha uingizaji wa vifaa vya mtandao na zana za mawasiliano," alisema.

Rais Kiir alisema hatua hiyo itaongeza  uingizwaji wa vifaa vya matumizi ya mtandao katika simu za mikononi  na kuongeza matumizi ya mitandao kwa wananchi.

"Msamaha wa kodi ninayopendekeza utafanywa kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato kuhakikisha njia za msamaha wa kodi zinaambatana na taratibu," alisema.

Alizitaka kampuni za simu za mkononi kupeleka  huduma za simu za mkononi kwa watu wa maeneo ya vijijini ili kuongeza idadai ya watu wanaunganishwa kwenye mitandao.

Alisema kuchelewa kuwaunganisha watu katika maeneo ya vijijini  kutadhoofisha juhudi za serikali za kuunganisha watu wake na wengine ulimwenguni kupitia teknolojia ya dijitali.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/93f76dec624d01bebc8d638b7dfdc2d5.jpeg

Katika hali isiyo ya kawaida, Mwanaume mmoja amekutana ...

foto
Mwandishi: JUBA 

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi