loader
Dstv Habarileo  Mobile
Wafanyakazi wa umma kuongezwa mishahara

Wafanyakazi wa umma kuongezwa mishahara

SERIKALI imetangaza kuwa watumishi wa umma kuanzia mwaka huu wa fedha watapata nyongeza ya mshahara kwa asilimia 100.

Akizungumza katika hotuba kwa taifa kwa njia ya televisheni juzi, Rais Salva Kiir aliiagiza Wizara ya Mafuta kutenga mapipa 5,000 ya mafuta yasiyosafishwa ili kukuza uchumi wa nchi hiyo na kuimarisha serikali kifedha kwa ajili ya kuhudumia wananchi pamoja na kuongeza mishahara.

Alisema anatambua wafanyakazi wamevumilia nyongeza ya mishahara kwa muda mrefu  kwani viwango vya mishahara havijabadilishwa tangu mwaka  2015

“Kuhusiana na suala hili, serikali imeamua kuongeza mishahara kufikia asilimia 100 katika bajeti ya mwaka huu  kama awamu ya kwanza na kuanza kutekelezwa mwaka huu wa fedha,” alisema.

Aidha, Rais Kiir aliahidi kutorudisha nchi tena kwenye vita vingine vya wenyewe kwa wenyewe.

"Ninawahakikishia kuwa sitawarudisha katika vita tena, tushirikiane katika kazi na kuhakikisha tunaleta maendeleo katika miaka ijayo," alisema.

Rais Kiir pia ametoa msamaha kwa wafungwa 15 ambao walikuwa wakitumikia vifungo katika magereza mbalimbali nchini.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Sudan Kusini, Riek Machar alisema wananchi wana matarajio makubwa kutoka kwa viongozi tangu nchi ilipopata uhuru muongo mmoja uliopita.

"Watu wetu wanatarajia mengi kutoka kwetu, ulimwengu pia unatarajia mengi kutoka kwetu, ili tuendelee kuwa kama ilivyo sasa, tunahitaji kuwa na amani kila wakati," alisema. 

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/5577be63ce24147cb55b8c61965a4049.jpeg

SERIKALI imetangaza kuwa watumishi wa umma kuanzia mwaka ...

foto
Mwandishi: JUBA

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi