loader
Dstv Habarileo  Mobile
Chididimo, Zuzu, mambo Mswano

Chididimo, Zuzu, mambo Mswano

MRADI wa Maji katika Mtaa wa Chididimo mjini Dodoma unatarajiwa kuanza rasmi mapema mwezi Agosti.

Hayo yamesemwa na Mbunge wa Dodoma Mjini, Anthony Mavunde katika ziara yake inayoendelea ndani ya jimbo hilo ya kuwashukuru wananchi kuichagua CCM 2020. Ziara hiyo anaongozana na kamati ya siasa ya CCM wilaya ya Dodoma mjini.

Aidha alisema mradi wa kusambaza  umeme maeneo yote ya mitaa iliyosalia katika kata ya Zuzu hasa mitaa ya Chididimo na Sokoine kufuatia fidia ya barabara ya mzunguko, bado malipo  kwa wananchi hayajahakikiwa na kuingizwa kwenye malipo.

Wakati huo huo, Mavunde alisema  anafuatilia kwa ukaribu malipo ya fidia kwa wananchi wanaopisha maeneo yao kwa ajili ya matumizi ya uwekezaji, mashamba darasa na hifadhi ya wanyama(Zoo)

Pia alisema atasimamia kuhakikisha sh milioni 20 za ujenzi wa miundombinu  ya vyoo katika shule ya Chididimo zinawasili mapema na kuanza utekelezaji wa  kujenga miundombinu hiyo.

Aidha Mavunde alisema atawekeza nguvu zaidi katika ujenzi wa Sekondari mpya kata ya Zuzu ambayo anaijenga kwa kushirikiana na wananchi ili kuwapunguzia mwendo watoto wa shule kutembea umbali mrefu.

Pia ametoa magodoro 30 kwa ajili ya  Hostel ya wanafunzi wa sekondari wanaotoka maeneo ya mbali.

Katika hatua nyingine, Mbunge huyo wa Dodoma mjini alisema atasaidia kuviwezesha vikundi vya wavuvi kurasimishwa na kuviwezesha mikopo vikundi vya wakina Mama,Vijana na watu wenye ulemavu.

 

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/e589f8a4cfddb0d744ff4731ed849653.jpg

MKUU wa Chuo cha Uhasibu Arusha ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi