loader
Dstv Habarileo  Mobile
Milioni 62 kuboresha Machinga Complex, marufuku Machinga barabarani

Milioni 62 kuboresha Machinga Complex, marufuku Machinga barabarani

SIKU chache mara baada ya Wafanyabishara waliopata maafa katika soko Kuu la Kariakoo kuhamishwa masoko ya Machinga Complex na Kisutu, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makala amesema kiasi cha shilingi milioni 62 zinahitaji kuboresha soko la Machinga Complex.

Hadi jana zaidi ya wafanyabishara 2054 walihamia katika masoko hayo huku  1,800 wamehamia katika soko la Machinga Complex  wakiwemo wafanyabishara wadogo wadogo (machinga)  570  na  Kisutu  ni 298  huku wengine wakiendelea kuongezeka  kwa mujibu wa Afisa masoko  wa jiji la Dar es Salaam ,Victor Rugemalila.

Makala aliyasema hayo mara baada ya kutembelea soko hilo na  lile la Kisutu kujua maendeleo ya wafanyabishara hao   na kuonekana kuwepo kwa changamoto la   paa ili kuzuia jua na mvua katika soko la Machinga Complex na kuwaahidi wafanyabiashara hao  kuwa atatumia ushawishi fedha zipatikane na uboreshaji utaanza wiki hii.

 “Nimefurahi kuona kuwa wengi wamepata maeneo ya kufanyia biashara  na mnaendelea na bishara zenu kama kawaida, na tuliwaahidi kuwa hamtalipia ushuru kwa muda wa miezi miwili kama sehemu ya kifuta machozi hilo tutazingatia,”alisema Makala.

Kwa upande wa soko la Kisutu alielekeza kuwa waliopewa maeneo ya kujenga fremu waruhusiwe kujenga na wasizungushwe na gharama zao ziwekwe wazi.

Pia aliielekeza Halmashauri ya Jiji la Ilala kuwaondoa Wafanyabiashara wanaoendesha biashara zao kwenye hifadhi za Barabara na kuwatafutia vizimba ndani ya Masoko hayo.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/9649c6fb88126d1383a22bcbf94032be.jpg

MKUU wa Chuo cha Uhasibu Arusha ...

foto
Mwandishi: Eveline Kitomari

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi