loader
Dstv Habarileo  Mobile
Katibu Mkuu Kilimo, atoa mwezi moja kukamilika Vihenge na Maghala

Katibu Mkuu Kilimo, atoa mwezi moja kukamilika Vihenge na Maghala

KATIBU Mkuu Wizara ya Kilimo, Andrew Massawe, ametoa mwezi mmoja kwa Menejimenti ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya chakula (NFRA) kuhakikisha mkandarasi UNIA SPZOO kutoka nchini Poland anamaliza kazi ya Ujenzi wa Vihenge na Maghala hayo ili yaweze kuanza kutumika.

Ameyasema hayo  alipotembelea na kukagua ujenzi wa mradi wa kuongeza uwezo wa kuhifadhi nafaka (Storage Capacity Expansion Project) katika eneo la Babati Mkoani Manyara.

Mradi huo ukikamilika utakuwa na uwezo wa kuhifadhi tani elfu arobaini na kwamba mpaka sasa  umefikia asilimia 99.8 .

Katika ziara hiyo Katibu Mkuu huyo aliongozana na Afisa Mtendaji Mkuu wa NFRA, Milton Lupa pamoja na baadhi ya wajumbe wa menejimenti ya wakala hiyo.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/1ca74f5858fb9102e84deb73e44364f5.jpg

MKUU wa Chuo cha Uhasibu Arusha ...

foto
Mwandishi: Frank Buliro

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi