loader
Dstv Habarileo  Mobile
Mtibwa, Coastal kazi ndio inaanza

Mtibwa, Coastal kazi ndio inaanza

BAADA ya kucheza Ligi Kuu kwa zaidi ya miaka 15 bila kushuka, Mtibwa Sugar leo ina kazi ya kujinusuru kutoshuka daraja katika mchezo wa kwanza wa mtoano dhidi ya timu ya Daraja la Kwanza, Transit Camp.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam na Jumamosi watarudiana katika dimba la Jamhuri, Morogoro kuamua hatma yake ya kubaki au kushuka.

Mtibwa imefikia hatua hiyo baada ya kushindwa kufanya vizuri kwenye ligi msimu huu wakimaliza katika nafasi ya 14 na kuangukia kapu la mtoano.

Klabu hiyo ya Morogoro ilianza kuyumba tangu msimu uliopita haikuwa na mwenendo mzuri.

Wanakutana na Transit Camp ambao walikuwa na msimu mzuri katika Ligi Daraja la Kwanza wakitoka Kundi B katika nafasi ya tatu.

Transit Camp inatafuta nafasi ya kupanda Ligi Kuu iwapo itaifunga Mtibwa katika michezo miwili.

Tayari Transit Camp walipita hatua ya awali ya mtoano baada ya kucheza na mshindi wa pili wa Kundi A African Sports na kuwatoa kwa mikwaju ya penalti 5-4 baada ya kila mmoja kushinda nyumbani kwake bao 1-0.

Mchezo mwingine utakuwa ni Coastal Union dhidi ya timu ya Daraja la Kwanza ya Pamba, utakaochezwa kwenye Uwanja wa Nyamagana, Mwanza na marudiano ni Jumamosi Mkwakwani, Tanga.

Coastal Union iliyokuwa inachezea kwe nye hatari ya kushuka daraja haikuwa vizuri na imenusurika dakika za mwishoni.

Timu hii ya Tanga imemaliza ligi katika nafasi ya 13 kwa pointi 40 nafasi ambayo anatakiwa kucheza mtoano kutetea kubaki Ligi Kuu.

Inacheza na Pamba iliyokuwa vizuri Ligi Daraja la Kwanza ikimaliza ligi katika nafasi ya pili kwenye Kundi B.

Pamba inayosaka nafasi ya kupanda Ligi Kuu kwa muda mrefu ina kazi mbele ya Coastal ambao wako tayari kupambana kwa uwezo wao wote kubaki.

Katika mchezo wa mtoano wa awali, timu hiyo ya Mwanza imeifunga Kengold iliyokuwa inashika nafasi ya tatu Kundi A na kuwatoa kwa penalti 4-3. Awali, Kengold ilishinda 2-0 ikiwa nyumbani kwao na mchezo wa marudiano, Pamba ikashinda 4-1.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/d13b2eee6aebc80ac6dc3431e77498de.jpg

AISHI Salum Manula sio jina geni ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi