loader
Dstv Habarileo  Mobile
Miradi ya bilioni 17/-  kuboresha maisha Segerea

Miradi ya bilioni 17/- kuboresha maisha Segerea

MBUNGE wa Jimbo la Segerea, Bonah Kamoli amesema miradi ya maendeleo inayotekelezwa jimboni humo yenye thamani ya Sh bilioni 17 itakuwa na manufaa makubwa kwa wananchi.

Kamoli alisema hayo alipokuwa katika ziara kwenye kata za Kinyerezi, Tabata na Buguruni kukagua maendeleo ya miradi hiyo, ikiwamo iliyo kwenye hatua za mwisho za ujenzi.

Alisema serikali imewezesha utekelezaji wa miradi hiyo jimboni humo ukiwamo wa  uendelezaji wa jiji la Dar es Salaam (DMDP), kituo cha daladala Kinyerezi na barabara ya Gongolamboto, yote ikiwa na thamani ya Sh bilioni 17.

 "Nimeanza ziara endelevu katika Jimbo la Segerea ya kutatua kero na kuangalia utekelezaji wa miradi ya serikali ambayo inajengwa. Naomba wananchi wa Segerea mtunze miradi yenu," alisema Kamoli.

 Akiwa katika mtaa wa Kifuru, kata ya Kinyerezi, wananchi waliomba ujenzi wa barabara ya NST Bangulo uharakishwe kwani wamekuwa wakipata shida hasa wakati wa masika.

 

Diwani wa Kata ya Kinyerezi, Leah Ng'itu aliomba wasaidiwe barabara za ndani kwa kuweka vifusi na kukarabati maeneo korofi kwenye barabara za lami. 

Naye, Diwani wa Kata ya Buguruni, Busoro Pazi alisema ujenzi wa mfereji katika mtaa wa Mvinjeni utakuwa suluhisho la kero ya mafuriko katika eneo hilo.

"Tunamshukuru Mbunge wetu kwa juhudi kubwa alizozifanya kuhakikisha katika mtaa wa Mivinjeni mfereji huu unajengwa, changamoto ya maji kutoka katika Mto Msimbazi kwenda kwenye makazi ya wananchi ilikuwa ni kubwa sana, lakini kupitia ujenzi wa mfereji kero hii itaisha kabisa," alisema Pazi.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/e79c75a09ccdceb160aae261e1b80b80.jpg

POLISI Mkoani Mtwara imikamata watu 15 kwa ...

foto
Mwandishi: Lucy Ngowic

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi