loader
Dstv Habarileo  Mobile
Tanzania yaibanjua Congo 1-0 U-23

Tanzania yaibanjua Congo 1-0 U-23

TIMU ya Taifa ya Tanzania chini ya miaka 23, imeanza vema michuano ya Cecafa Challenji baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0  lililofungwa na mshambuliaji Reliants Lusajo aliyetumia vema krosi ya Nickson Kibabage mchezo uliochezwa katika Uwanja wa Bahir Dar, nchini Ethiopia.

Tanzania walipata bao la pekee katika dakika ya 66 baada ya jitihada binafsi za mlinzi wa kushoto wa Tanzania, Nickson Kibabage kuitambuka ngome ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kisha kupiga krosi iliyomkuta Lusajo aliyeandika bao la ushindi.

Mchezo huo ulikuwa na presha kubwa kwa  kila timu kufanya mashambulizi ya kushtukiza, lakini hadi dakika 45 za kipindi cha kwanza zinatamatika,  hakuna timu iliyokuwa imeona lango la mwenzake, kipindi cha pili Congo, walifanya mashambulizi makali katika lango la Tanzania, lakini uimara wa mlinda mlango Metacha Mnata ulikuwa kikwazo kwao.

Kwa matokeo hayo, Tanzania imepata pointi tatu sawa na Uganda hivyo Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuondolewa katika michuano hiyo wakiwa hawana pointi hata moja.

Tanzania inatarajiwa kucheza mchezo wake wa pili dhidi ya Uganda, mchezo unaotarajiwa kupigwa kesho katika Uwanja wa Bahir Dar, ili kutafuta nafasi ya kumaliza kinara katika Kundi A.

Wakati huohuo, mchezo wa mapema timu ya Taifa ya Kenya imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Sudan Kusini mchezo uliopigwa katika Uwanja wa Bahir Dar.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/c0222d3f1ec5eecb699bdff9999c2efc.jpg

AISHI Salum Manula sio jina geni ...

foto
Mwandishi: Martin Mazugwa

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi