loader
Dstv Habarileo  Mobile
Mtibwa matumaini, Coastal yabanwa

Mtibwa matumaini, Coastal yabanwa

KLABU ya soka ya  Mtibwa Sugar imeonesha matumaini ya kubaki Ligi Kuu msimu ujao, baada ya kushinda mchezo wa kwanza wa mtoano dhidi ya Transit Camp, huku Coastal Union ikibanwa ugenini dhidi ya Pamba.

Katika mchezo huo uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, Mtibwa ilishinda mabao 4-1 dhidi ya Timu ya Daraja la Kwanza Transit Camp na kubakiza matumaini ya kuendelea kuwepo.

Mabao yalifungwa na Ibrahim Ahmada matatu dakika ya (9, 70, 84), Kelvin Sabato dakika ya 12 na kuifanya Mtibwa kuondoka kifua mbele kwa idadi kubwa ya mabao  huku la Transit likifungwa na Karegea Hazanga dakika ya 16.

Kwa ushindi huo, Mtibwa inahitaji matokeo ya sare au ushindi wowote katika mchezo wa marudiano utakaochezwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro ili kuendelea kucheza msimu ujao.

Kwa upande wa Coastal Union imebanwa ugenini dhidi ya timu ya Daraja la Kwanza ya Pamba kwa matokeo ya sare ya mabao 2-2 katika mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Nyamagana, Mwanza.

Coastal ilitangulia kupata bao la uongozi dakika ya kwanza lililofungwa na Abdul Suleiman na dakika ya 12 James Ambrose alisawazisha. Dakika ya 77 wakapata bao la pili la penalti likifungwa na  Emanuel Haule kabla ya Coastal kusawazisha dakika ya 88 kupitia kwa Raizin Hafidh.

Pamba FC walikosa mkwaju wa penalti uliopigwa na Elinywesya Simbu katika dakika ya tano baada ya  nahodha wa timu hiyo, Majaliwa Shaban kuangushwa  eneo la hatari.

Mchezo wa marudiano wa Coastal na Pamba utakaochezwa Jumamosi mkoani Tanga ndio utakaoamua wa kubaki au kupanda.

Coastal ikipata sare tasa,  bao 1-1 au  ushindi wowote atakuwa na nafasi ya kubaki msimu ujao au Pamba inahitaji ushindi kuanzia bao 1-0 na kuendelea kujihakikishia nafasi ya kupanda Ligi Kuu.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/592142a3fdacc8d8a150cbba2a9f00cb.jpg

MKUU wa Chuo cha Uhasibu Arusha ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi