loader
Dstv Habarileo  Mobile
CCM Mtwara yampongeza Rais Samia 'Tozo Miamala ya Simu'

CCM Mtwara yampongeza Rais Samia 'Tozo Miamala ya Simu'

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mtwara kimempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa hatua aliyochukua ya kutoa maelekezo kwa wizara ya fedha kutafuta suluhu kuhusu malalamiko ya wananchi kwenye viwango vya tozo ya miamala.

Katibu wa CCM Mkoa wa Mtwara, Alhaji Saad amesema hayo leo na kuongeza kuwa chama hicho kinamuunga mkono na kusema kuwa hatua hiyo ya Rais inaashiria kuwa Rais anazingatia matakwa ya chama ambayo yanaelekeza kiongozi yeyote awa anasikiliza kero na changamoto zinaziwakanili wananchi wake anaowaongoza.

“Chama cha Mapinduzi Mkoa tunampongeza na kumuunga mkono muheshimiwa Rais kwa hatu aliyoichukua ya kusikiliza kilio cha wanyonge ambacho kwa mda mrefu wamekuwa wakilalamika kuhusu tozo za miamala ya sim,” amesema.

Saad amesema hatua hiyo ya Rais ni hatua ya kiungwana ambayo ameonyesha yupo karibu na watanzania na anawasikiliza.

“Kimsingi tunamshukuru sana na kumpongeza. Tunamuomba mwenyezi Mungu aendelee kumpa  hekima na busara aendelee kuwatumikia watanzania kama tulivyokuwa tunatarajia wanachama wa chama cha mapinduzi,” amesema.

Kwa hatua nyingine chama hicho kimesema kinaunga mkono Rais kwa kuruhusu wananchi wachome chanjo kwa hiari yao kitendo ambacho cha kuungwa mkono hatua hiyo.

Rais aliagiza Wizara ya Fedha na Mipango itafute suluhu ya malalamiko ya wananchi kuhusu viwango vya tozo ya miamala ya simu iliyo anza tarehe 15 Julai 2021, ikiwa ni utekelezaji wa Sheria ya Fedha iliyopitishwa na Bunge la Bajeti.

 

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/cb5f29a327f80d18b5a8d8baa1d0a2de.jpeg

POLISI Mkoani Mtwara imikamata watu 15 kwa ...

foto
Mwandishi: Na Anne Robi, Mtwara

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi