loader
Dstv Habarileo  Mobile
Mpango: Hakikisheni fedha hazipotei

Mpango: Hakikisheni fedha hazipotei

MAKAMU wa Raisi Dk Philip Mpango amewataka viongozi katika ngazi za mkoa na halmashauri zote katika Mkoa wa Mtwara, kusimamia fedha zilizopelekwa na serikali mkoani humu kwa ajili ya maendeleo ya wananchi kwa kuhakikisha haipotei hata shilingi moja.

Akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Newala, Dk Mpango aliwataka viongozi wa mkoa huo kuwa kuhakikisha haipotei hata shilingi moja katika fedha hizo za maendeleo.

“Nimewasikia wabunge wakimshukuru Mheshimwa Rais (Samia Suluhu) na serikali nzima kwa kuleta fedha nyingi kwa wilaya yetu ya Newala kwa shughuli mbalimbali, nataka niwaombe tena viongozi katika ngazi ya mkoa na ngazi ya wilaya na halmashuri zote kusimamia fedha vizuri isipotee hata shilingi moja, sasa ikipotea...,” alisema.

Alisema hatasita kuchukua hatua kwa mtumishi yeyote atakayebainika kutosimamia vyema fedha za wananchi wakiwemo wakulima wa korosho. “Nilianza jana (juzi) pale Nanyumbu, niliagiza yule mkurungezi akae pembeni (Hamisi Dambaya), kwamba amejenga stendi ya Sh bilioni 2.25, haifanani kabisa na hizo fedha,”alisema.

Makamu wa Rais alimwagiza Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Marco Gaguti na wakuu wa wilaya zote mkoani humo pamoja na Wizara ya Kilimo na Bodi ya Korosho Tanzania (CBT) kuhakikisha fedha za wakulima na wananchi, wote zinasimamiwa vizuri.

Juzi Dk Mpango alifanya ziara ya kushtukiza katika Stendi ya Mabasi ya Mangaka iliyopo Wilaya ya Nanyumbu mkoani Mtwara na kumuagiza Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi, Dk Festo Dugange kumsimamisha kazi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Nanyumbu, Hamis Dambaya ili kupisha uchunguzi kutoka vyombo husika. Mpango alitoa uamuzi huo kutokana na kukasirishwa na uongozi wa wilaya kutokana na matumizi makubwa ya fedha yasiyolingana na matokeo ya ujenzi wa mradi.

Kwa mujibu wa taarifa aliyopokea Dk Mpango, ujenzi wa majengo ya stendi hiyo umetumia Sh bilioni 2.2 kiasi ambacho Makamu wa Rais alisema hakilingani na ujenzi huo.

foto
Mwandishi: Na Anne Robi, Mtwara

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi