loader
Dstv Habarileo  Mobile
Kikwete asikitishwa moto bweni la wasichana

Kikwete asikitishwa moto bweni la wasichana

TUKIO la moto kuunguza bweni la wasichana katika Shule ya Sekondari Kiwangwa iliyopo Bagamoyo mkoani, limemsikitisha Rais wa Awamu ya Nne Jakaya Kikwete aliyefanikisha ujenzi wa bweni hilo akiwa mbunge.

Akizungumza baada ya kutembelea shule hiyo, Kikwete alisema tukio hilo linasikitisha. Alisema akiwa mbunge mwaka 1990 hadi mwaka 2005 alifanikisha kuanzishwa kwa shule nne za sekondari ikiwamo ya Kiwangwa. “Katika ujenzi wa bweni hili nilitafuta saruji nikafyatua matofali, vijana wakaja hapa wakaweka kambi ujenzi ukaanza nikamwomba Sabodo (Mfanyabiashara Jaffar) akajenga bweni la wasichana nalo likaungua nasikitika sana kwanini ya wasichana,” alisema Kikwete.

Aidha alisema shule ambazo alihamasisha ni Sekondari ya Lugoba, Kikaro na Mandela. “Lugoba nako nilimuomba Shubhash Patel (mfanyabiashara) atujengee bweni la wasichana nalo liliungua, yanaungua ya wasichana tu sisemi na ya wanaume yaungue, ila inashangaza lakini ndiyo ajali na imeshatokea,” alisema.

Alibainisha kuwa kwa sasa kilichobaki ni kujenga bweni hilo ili wanafunzi watoke kulala kwenye madarasa na kulala kwenye bweni, uchunguzi ufanyike na majibu yawe sehemu ya kukabiliana na moto shuleni hapo. “Hii ni kazi ya mbunge, mimi nilijenga nikiwa mbunge na sasa mbunge wenu ajenge halmashauri mpo diwani yupo tupambane ili kurudisha bweni kwenye hali yake ya kawaida,” alisema Kikwete.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chalinze, Ramadhan Posi alisema wamejipanga kuhakikisha ujenzi unafanyika ili wanafunzi warudi kwenye bweni.

foto
Mwandishi: Na John Gagarini, Bagamoyo

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi