loader
Dstv Habarileo  Mobile
Huawei kuwekeza  dola mil 150 kukuza vipaji vya kidijiti

Huawei kuwekeza dola mil 150 kukuza vipaji vya kidijiti

KAMPUNI ya Huawei imepanga kuwekeza Dola za Marekani milioni 150 katika kukuza vipaji vya dijiti katika kipindi cha miaka mitano ijayo.
Mpango huo unatarajia kuwanufaisha vijana milioni tatu.

"Leo tunatangaza mwendelezo wa mpango wa kizazi kijacho cha Huawei (Huawei's Seeds for the Future Program 2.0.) kama sehemu ya ahadi yetu ya kuendelea kukuza vipaji. Tutawekeza Dola milioni 150 katika mpango huu kwa kipindi cha miaka mitano ijayo na kusaidia wanafunzi wa vyuo vikuu na vijana kuboresha ujuzi wao wa dijiti. Programu hii inatarajiwa kuwanufaisha watu milioni tatu," alisema Mwenyekiti wa Huawei, Liang Hua.


Hua alisema Huawei ilianza kupanua programu zake za kukuza vipaji kupitia ufadhili wa masomo mwaka 2008 pamoja na mashindano ya teknolojia na mafunzo ya ustadi wa dijiti.

Alisema katika programu hizo iliwekeza zaidi ya Dola milioni 150 za Marekani na kunufaisha watu zaidi ya milioni 1.5 kutoka nchi zaidi ya 150 ulimwenguni.

Kwa mujibu wa Hua, mpango huo unakusudia kukuza vipaji vichanga kutoka kote ulimwenguni, kuwapa mafunzo kuhusu teknolojia ya kisasa ili kuwasaidia kukuza ujuzi na fikra za ushindani katika mazingira ya kazi ya siku zijazo.

Alisema Huawei ilianzisha programu hiyo barani Afrika mwaka 2014 na imewanufaisha wanafunzi 2,000 kutoka nchi zaidi ya 25 za Afrika na kuongeza kuwa mpango huo na juhudi za Huawei katika kukuza vipaji vya ICT vimetambuliwa na serikali nyingi za Afrika.
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk Leonard Akwilapo, alisema mpango  huo ni muhimu katika kukuza ujuzi wa kuajiriwa.

"Mpango huu unadumisha ushirikiano kati ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Huawei Tanzania katika kukuza mahusiano endelevu ya rasilimali watu katika ICT. Programu hii inafanya kazi kama daraja ambalo linaziba pengo kati ya mafunzo ya kinadharia na mahitaji ya vitendo katika soko la ajira," alisema Dk Akwilapo.

Makamu Rais wa Huawei Kanda ya Kusini mwa Afrika, Yang Chen, alisema Huawei imejitolea kwa maendeleo ya rasilimali watu Afrika.
“Afrika ina idadi kubwa ya vijana. Vijana hawa ndiyo rasilimali kubwa ya Bara hili ambayo itaimarisha uchumi katika siku zijazo.

Huawei inashirikiana na serikali za Afrika, taasisi za elimu na tasnia ili kuwapa viongozi wa siku zijazo maarifa ya kisasa katika kiwango cha juu ulimwenguni pamoja na fursa ya kutumia maarifa hayo kuleta maendeleo barani humo," alisema Chen.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/c8253c26230b0526a2b81b2c3e20134e.jpeg

SHIRIKISHO la Wafanyabiashara na wenye viwanda nchini ...

foto
Mwandishi: BEIJING, China

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi