loader
Dstv Habarileo  Mobile
Afrika ina haja ya kuwaogopa mabeberu?

Afrika ina haja ya kuwaogopa mabeberu?

KWA muda mrefu sana historia ya Afrika imefichwa machoni mwa wana-asilia na mabeberu waliolitawala bara hili kwa karne kadhaa zilizopita. Historia hii imechangia kwa kiasi kikubwa kufifisha ukweli kuhusu ustaarabu na maendeleo ya Afrika na hasa Tanzania kama chanzo cha ustaarabu ulimwenguni.

Wakati nchi kama Nigeria na nyinginezo za Afrika ya Kati zimebakiza tawala za kikoloni na zile za kimila, mataifa mengine ya Afrika yametupilia mbali tawala hizi.

Ni wazi kwamba kufanya hivi kumesababisha kwa kiwango kikubwa kupoteza asili yetu, Imani zetu na hata ukweli kuhusu nguvu zetu tulizonazo kama waafrika.

Wakati Wajerumani, Wachina na wengineo wakija Tanzania hasa Tabora kuhiji kwenye kaburi la mtu aliyeishi zaidi ya miaka 312 kwenye familia ya kichifu ya Mtemi Milambo, sisi tunaona kufanya hivyo ni kukufuru na kupotoka. Ni wapi iliandikwa hiyo? Hakuna awezaye kueleza vyema.

Mpenzi msomaji, ukisoma maandiko matakatifu yanasema, Mungu aliumba bustani ya Edeni na kisha kuweka kila kitu kwa ajili ya mwanadamu aliyeumbwa aishi bila taabu yoyote. Alimwekea kila kitu ambacho anahitaji.

Kila nikisoma maandiko haya hupiga taswira ya nchi yangu Tanzania na Bara la Afrika kisha kuangalia utajiri tulionao na jinsi tusivyoutumia kwa maslahi mapana ya wananchi wake.

Katika filamu ya black panther inaonesha jinsi ambavyo taifa mojawapo la Afrika ambalo halionekani kwa macho ya kawaida lina miliki utajiri mkubwa sana lakini kuingiliwa na wageni kunasababisha kuiba teknolojia yake na kuitumia vibaya.

Msomaji wa makala haya, ukikaa na machifu wa taifa hili ambao kimsingi wanaonekana kusahaulika utagundua mengi sana kuhusu utawala wa Bara la Afrika. Utagundua kwamba Mungu amebariki bara hili na kwamba historia ya nchi zetu za Afrika ilibadilishwa kwa maslahi ya kuendelea kututawala.

Kama historia bado inamilikiwa na wazee hawa, kwanini tusiwatumie katika kuandika upya historia ya bara letu la Afrika? Tunaona aibu ya nini juu ya asili yetu?

Ni wazi kwamba nchi zetu zimebarikiwa kila mmea ulioumbwa na Mungu. Miti hii ya kila aina tulipewa itusaidie kwa tabibu za kila siku. Hata hivyo, kutokana na ukoloni tumetupilia mbali asili yetu na kuanza kutegemea ubeberu mtupu.

Miti iliyopo inaweza kutibu kila aina ya ugonjwa unaoonekana na ambao haujatokea bado. Ya nini tusitumie mitishamba yetu kujitibu kwa kuzingatia asili yetu? Kwani ikiboreshwa na kuendana na teknolojia iliyopo sasa na kuanza kutumika itatudhuru nini sisi Waafrika na wengine wanataotumia?

Upo mfano mzuri wa ndugu zetu Wachina ambao wameweka nguvu kubwa katika kutengeneza na kutumia dawa wanazozitengeneza wenyewe kwa mitishamba ya asili walionayo katika nchi yao.

Juzi, niliona habari kwamba Marekani inatoa msaada wa chanjo za J&J kwa mataifa maskini na Afrika ikiwemo! Nikajiuliza maswali mengi. Moja ya swali ni kwamba, mataifa ya Marekani, Afika Kusini, Uingereza pengine na mengineyo yamezuia utumiaji wa chanjo hizo (si zote) baada ya kugundua zina hitilafu ya kuganda kwa damu kwenye ubongo wa binadamu.

Bila shaka hatua za uchunguzi wa kujiridhisha zimefanywa na serikali yetu kwa usalama wa chanjo hizo na binafsi ningetamani kusikia kauli ya uhakika wa chanjo hizo kwa afya za wananchi unazingatiwa kuliko kitu chochote.

Usalama huo uondoe maswali ya wananchi kwa hofu yoyote walionayo kuhusu usalama wao na kuiamini serikali katika hilo kwamba si jambo linalohatarisha maisha ya watu kwa namna yoyote ile na mpango uwe kuwa na chanjo yetu wenyewe Waafrika na Watanzania ikibidi.

Bara letu lina madini ya kila aina; lina wanyama karibia aina zote duniani; lina milima, mito, ardhi yenye rutuba na watu wenye maarifa makubwa waliosambaa duniani kote. Ni vyema kutumia rasilimali hizi kujitegemea na kuendesha mambo yetu wenyewe kwa maslahi yetu kama Waafrika.

Hatua hii itatusaidia kukomaa katika kujitegemea kwenye mambo mengi na kuondoa utegemezi ambao hatari yake wakati mwingine ni kutuingiza kwenye mikono ya ukoloni kwa njia mpya (ukoloni mamboleo).

Ni ukweli kwamba, pamoja na kukua kwa sayansi na teknolojia, mabeberu hawajaacha asili yao hata kidogo. Mataifa kama China, pamoja na teknolojia mpya, yanaendeleza na kurithishana asili na tamaduni zao! Kwanini waafrika tuache zetu?

Utajiri na hazina Afrika iliyo nayo haihitaji msaada wowote kutoka ulaya au Amerika. Kinachotuharibu ni kutoruhusu hazina yetu kutuepusha na kila jambo kwa Imani zetu.

Mfano ukiachilia mbali historia ya kupikwa iliyoandikwa na mkoloni, ukweli unaonesha kwamba shujaa wa ulimwengu kabla ya wale wanaosomwa kwenye vitabu vya historia, ni Mtemi Milambo ambaye alipambana na Napolean na kumshinda, Mau wa China na kumshinda, waarabu na hata wajerumani.

Upiganaji wake ulikuwa wa ajabu sana. Alikuwa jemedari wa vita aliyebobea kwa kila namna. Alipata nguvu za mabibi na mababu zake na jeshi lake la warugaruga lililokuwa limeimarika kwa kila namna. Ushujaa wake ulijulikana ulimwenguni kote.

Taarifa zinaonesha kwamba Milambo alipopigana na Mau wa China na kumshinda, alivua pete na kumkabidhi kwa heshima ya ushujaa wake. Ni wazi kwamba kizazi chake hadi sasa kipo. Kama Taifa la Tanzania tunawaza nini juu ya kufanya historia hii ifahamike ulimwenguni kote?

Ndugu msomaji, Makala yangu ya leo ilikuwa na lengo kuamsha fikra zetu  Waafrika na kuanza kuhamasisha na kuinua asili yetu; kutumia asili yetu katika kukabili mambo yetu na kutumia vitu vyetu ya asili katika kukabiliana na changamoto za kiulimwengu. Mungu azidi kutulinda, kutubariki na kutuondoa katika utumwa wa ukoloni mambo leo.

Mwandishi wa Makala haya ni mchangiaji wa gazeti hili na anapatikana kwa mawasiliano; 0712246001; flugeiyamu@gail.com

                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                    

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/8e29e490c3f166a07953d45a0e9e0f99.jpeg

OFISI ya Taifa ya Ukaguzi (NAOT) ni Taasisi ...

foto
Mwandishi: Felix Lugeiyamu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi