loader
Dstv Habarileo  Mobile
Dk. Msolla: Yanga tulieni

Dk. Msolla: Yanga tulieni

MWENYEKITI wa klabu ya Yanga Dk. Mshindo Msolla, amewataka mashabiki wa timu hiyo kuwa watulivu kipindi hiki cha mapumziko huku yeye na viongozi wenzake wakipambana kuimarisha kikosi chao cha msimu ujao.

Yanga licha ya kutobeba taji lolote la ndani msimu wa mwaka 2020/21 lakini imekuwa na mafanikio makubwa msimu huu, baada ya kumaliza nafasi ya pili kwenye michuano yote mikubwa ya ndani ambayo ni Ligi Kuu ya Tanzania Bara na Kombe la FA huku watani zao Simba wakibeba mataji yote mawili.

Akizungumza na gazeti hili jana, Dk. Msolla alisema pamoja na kushindwa kutimiza malengo yao kwa kubeba mataji hayo, lakini wanafarijika na ushindani uliooneshwa na kikosi chao.

“Malengo yetu ya kwanza ilikuwa ni kubeba mataji ya Ligi Kuu na Kombe la FA, lakini imeshindikana kwa kiwango kidogo sana tunajivunia uimara wa kikosi chetu lakini tunakwenda kwenye dirisha la usajili tumejipanga kukiboresha kikosi chetu kwa kusajili wachezaji ambao wataimarisha sehemu zenye mapungufu ili msimu ujao tuweze kutimiza ahadi yetu,” alisema Dk. Msolla.

Kiongozi huyo alisema, kabla ya msimu uliopita kumalizika tayari walishaanza mchakato wa usajili kwa kushirikiana na kocha wao Nasredine Nabi, na mpaka sasa kuna baadhi ya wachezaji wameshamalizana nao hivyo hiyo ni dalili tosha kwamba msimu unaokuja hautokuwa wa mzaha kwao.

Alisema uongozi wa Yanga kwa kushirikiana na wahisani wao GSM, wamekuwa wakipambana kuhakikisha timu hiyo inakuwa bora msimu ujao ndio maana amewataka mashabiki wao kuendelea kuwa watulivu kipindi hiki cha usajili ili wafanikishe walichokikusudia.

Dk. Msolla alisema wamekuwa makini kwenye usajili wa safari hii ndio maana wamefanya siri kutanganza wachezaji ambao wamemalizana nao lakini mchakato huo unakwenda vizuri na umekamilika kwa asilimia 90 kwa kuzinasa saini za wachezaji wanaowahitaji.

Mpaka sasa Yanga imeshakamilisha usajili wa beki wa kulia wa AS Vita Djuma Shabani huku uongozi ukiendelea kukamilisha taratibu za wachezaji wengine ambao imekusudia kuwasajili msimu huu.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/5985609df816c097b7b2e1fb20a6c246.jpg

NYOTA wa zamani wa Yanga, Charles Bonifasi Mkwasa ...

foto
Mwandishi: Mohamed Akida

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi