loader
Dstv Habarileo  Mobile
Yanga kushusha nyota wapya Kagame

Yanga kushusha nyota wapya Kagame

KIKOSI cha wachezaji 23 cha Yanga wakiwemo wachezaji sita wapya kitaingia kambini kesho Ijumaa kujiandaa na michuano ya Kagame itakayoanza Agosti 1-15 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Katika michuano hiyo, Yanga imepangwa Kundi C pamoja na timu za Express ya Uganda na Nyasa Big Bullets ya Malawi ambayo ni timu mualikwa kwenye michuano hiyo.

Akizungumza na HabariLEO jana, Meneja wa timu hiyo, Hafidh Salehe alisema maandalizi yote kwa ajili ya kambi hiyo yamekamilika na wachezaji wataanza kuripoti kambini Avic Town Kigamboni kesho mchana.

Alisema mbali na wachezaji sita wapya, pia watatumia wachezaji saba kutoka kwenye kikosi chao kilichoshiriki Ligi Kuu na kumaliza nafasi ya pili, pamoja na wachezaji 10 kutoka kwenye timu yao ya vijana wenye umri wa miaka 20.

“Tumeamua kutumia kikosi mchanganyiko ili kuwapa mapumziko baadhi ya wachezaji wa kikosi cha kwanza kutokana na kutumika mfululizo kwenye msimu ulio malizika hivi karibuni na kutoa nafasi kwa wale ambao hawakupata nafasi ya kucheza mechi nyingi,” alisema Hafidhi.

Meneja huyo alisema kambi yao itaendelea kubaki Avic Town Kigamboni na wachezaji wanatarajiwa kuripoti kesho mchana kwa ajili ya kuanza mazoezi.

Alisema kwa upande wa wachezaji wapya, baadhi yao wameshaarifiwa na uongozi wa juu na wengine wanatarajiwa kuwasili nchini wakati wowote kwa ajili ya kuungana na wenzao kwa ajili ya michuano hiyo.

Hafidhi alisema pamoja na kuchanganya kikosi, lengo lao kubwa ni kutwaa taji hilo na kuwaanda wachezaji wao kabla ya kuanza maandalizi ya msimu ujao ambao wamedhamiria kufanya vizuri zaidi.

Kiongozi huyo pia alilizungumzia Kundi C ambalo wamepangwa, akisema ni lenye timu ngumu ambazo zitawapa kipimo kizuri wachezaji wao hasa wapya ilio wasajili ili kuona ubora wao katika kuipigania timu hiyo.

Hafidhi alisema wameshawahi kucheza na timu hizo kwa nyakati tofauti, hivyo wanajua uwezo wao na watahakikisha wanacheza kwa malengo ili kulibakisha taji hilo kwenye aridhi ya Tanzanaia.

Yanga inashika nafasi ya pili kwa kulitwaa taji hilo la Kagame mara tano ambapo watani wao Simba ambao ndio wanaoongoza Afrika Mashariki na Kati kwa kulibeba mara sita.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/4880638cf0b23e2867f1baba31372b79.jpg

NYOTA wa zamani wa Yanga, Charles Bonifasi Mkwasa ...

foto
Mwandishi: Mohamed Akida

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi