loader
Dstv Habarileo  Mobile
Riadha tayari kusaka medali Olimpiki 2020

Riadha tayari kusaka medali Olimpiki 2020

TIMU ya Tanzania itakayoshiriki Michezo ya 32 ya Olimpiki ya 2020 Tokyo, Japan inaondoka leo na iko tayari kutwaa medali katika michezo hiyo iliyoanza Julai 23 na itafanyika hadi Agosti 8.

Tanzania katika michezo hiyo iliyoahirishwa mwaka jana kutoka na covid-19, ina wakilishwa na timu pekee ya riadha yenye wachezaji watatu wa mbio za marathoni, Alphonce Simbu, Gabriel Geay na Failuna Abdi.

Kocha Mkuu wa timu hiyo, Thomas John alisema jana kuwa, wachezaji hao wapo katika ari kubwa na wanakwenda kushinda ila aliwataka Watanzania kuwasapoti.

Alisema wamejiandaa kwenda kushindana na wanajua watakutana na ushindani mkubwa kwani kila mtu ametoka katika nchi yake kwenda Japan kuwania medali ya dhahabu, fedha au shaba.

Nahodha wa timu hiyo, Simbu alisema wamejiandaa vizuri na wako tayari kwa safari hiyo leo alasiri wakitoka Dar es Salaam kupitia Dubai hadi Tokyo, Japan.

Alisema wamejiandaa vizuri na wachezaji siku zote hawakosi majeraha madogo madogo na hata yeye anayo, lakini hayawezi kuwa kikwazo kwake kufanya vizuri, kwani amejipanga vizuri kuhakikisha anafanya vizuri.

Simbu katika Olimpiki ya Rio de Jeneiro 2016 nchini Brazil, nusura apate medali baada ya kumaliza watano kwa kutumia muda wa saa 2:11:15.

Alisema tayari wamepimwa mara mbili covid-19 na wote wako vizuri tayari kwa safari hiyo kwenda kuwania medali katika michezo hiyo mikubwa kabisa duniani inayoshirikisha mchezo mbalimbali.

Aliwahakikishia Watanzania kuwa timu yao itapambana na kufanya vizuri licha ya uchache wao ikilinganishwa na nchi nyingine ambazo zimepeleka wachezaji wengi na michezo tofauti tofauti.

Tanzania ilianza kushiriki Michezo ya Olimpiki mwaka 1968 Mexico na ilipata medali za kwanza Moscow, Urusi 1980 kupitia kwa Filbert Bayi na Suleiman Nyambui katika mbio za meta 3,000 kuruka viunzi na maji na 5,000.

Daktari wa timu hiyo, Mwanandi Mwankemwa alisema jana kuwa hakuna mchezaji mwenye matatizo ya afya, kwani wote wako fiti na tayari kwa safari na michezo hiyo.

Akielezea zaidi, Mwankemwa alisema timu hiyo itafika Tokyo kesho Julai 30 na siku moja baadae itapanda ndege kwenda katika Kisiwa cha Sapporo, ambako marathoni itafanyikia huko Agosti 7 na 8 kwa wanawake na wanaume.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/24afcd72b802897f0316d88dce6d2e92.jpg

NYOTA wa zamani wa Yanga, Charles Bonifasi Mkwasa ...

foto
Mwandishi: Cosmas Mlekani

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi