loader
Dstv Habarileo  Mobile
Mwanadiplomasia wa uchumi aipa mbinu ya masoko Tantrade 

Mwanadiplomasia wa uchumi aipa mbinu ya masoko Tantrade 

MKURUGENZI wa Idara ya Diplomasia ya Uchumi, Balozi Edwin Rutageruka ametoa wito kwa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tantrade) kuimarisha Kitengo cha Intelijensia ya Masoko cha mamlaka hiyo ili kishirikiane na  waambata wa biashara kwenye Balozi za Tanzania kwenye nchi mbalimbali.

Balozi Rutageruka ambaye alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade, alitoa ushauri huo juzi wakati akikabidhi ofisi kwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo,  Latifa Khamis.

Alisema ndoto yake ilikuwa kuifanya TanTrade kuwa na chanzo cha mapato zaidi ya kimoja na kumshauri Latifa kusimamia ukamilishwaji wa miradi ya maendeleo kikiwamo Kituo cha Nafaka cha Gairo mkoani Morogoro, Kilimanjaro Business Park mkoani Kilimanjaro na Kurasini Export House, Dar es Salaam.

Miradi mingine aliyoitaja ni Kituo cha Biashara cha Wajasiriamali, mradi wa kuendeleza Uwanja wa Maonesho wa Mwalimu Nyerere (SabaSaba), pamoja na kusimamia ujenzi wa mradi wa Uwanja wa Maonesho ya Kimataifa uliopo Fumba, Zanzibar.

Pia aliitaka Tantrade kusimamia miradi ya uwezeshaji biashara nchini ukiwamo wa Tanzania Trade Information Portal, Tanzania Spice Label na wa E-Shop wa Shirika la Posta.

Kwa upande wake, Latifa aliwataka wafanyakazi wa TanTrade kufanya kazi kwa uadilifu na ushirikiano ili kuiwezesha mamlaka hiyo kujenga mazingira wezeshi ya biashara nchini.

Alisema kufanya kazi kwa bidii kutawezesha kufikia malengo yaliyokusudiwa kwa wakati na kuwaonya wenye tabia ya uvivu na uzembe.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/a55a22b2402799075e8d8c1f2425a7b7.jpeg

SHIRIKISHO la Wafanyabiashara na wenye viwanda nchini ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi