loader
Dstv Habarileo  Mobile
Vijana wahamasishwa  kusoma taaluma ya forodha 

Vijana wahamasishwa kusoma taaluma ya forodha 

VIJANA wametakiwa kuchangamkia kusoma taaluma ya forodha na kodi kwani inahitajika zaidi kipindi hiki ambacho Tanzania inaendelea kukuza mapato ya ndani ili kupunguza utegemezi.

Ofisa Uhusiano wa Umma wa  Chuo cha Kodi (ITA), Oliver Njunwa alitoa rai hiyo kwenye Maonesho ya 16 ya Elimu, Sayansi na Teknolojia yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es salaam.

Alisema kutokana na kuhitajika kwa taaluma hiyo, vijana wanaohitimu katika chuo hicho wanakuwa msaada mkubwa katika ukusanyaji wa mapato ya ndani.

Alisema katika kipindi cha maonesho hayo wanawasaidia wanaotembelea banda la chuo hicho kuchagua kozi inayowafaa kutokana na sifa walizonazo na kama hawana sifa za kujiunga wanawaelekeza katika vyuo vingine.

Njunwa aliwaondoa hofu  wanaodhani wakisoma chuo hicho ni lazima wafanye kazi Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) hivyo kuwapo ufinyu wa ajira, kwani kuna fursa nyingine nyingi za kufanya kazi ambazo mhitimu anazipata.

Alisema chuo hicho kinatoa mafunzo ya umahiri katika usimamizi wa forodha na kodi ngazi ya astashahada, stashahada na shahada.

Alisema pia kinatoa stashada ya uzamili katika kodi na kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Chuo cha Muenster cha Ujerumani kinatoa shahada ya uzamili katika sheria ya kodi na usimamizi.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/ad8c26ca3f0a4aa6f233cf5313f83072.jpg

WASICHANA waliopata ujauzito katika umri mdogo ...

foto
Mwandishi: Lucy Ngowi

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi