loader
Dstv Habarileo  Mobile
Urusi yashtushwa na shughuli za Marekani katika eneo lake

Urusi yashtushwa na shughuli za Marekani katika eneo lake

MSEMAJI wa Ikulu ya Urusi Dmitry Peskov amesema nchi yake imeshtushwa na shughuli za kiusalama za Marekani katika eneo lake.

Hata hivyo, Peskov alikataa kulinganisha mafanikio ya mashirika ya usalama ya nchi hizo mbili.

“Shughuli maalumu za kiusalama za Marekani zinafanyika katika eneo letu, kwa kweli hii ni hali ya kutia wasiwasi,” alisisitiza na kuongeza kuwa hali hiyo imekuwa ikitokea mara kwa mara na bado inaendelea.

Peskov alihojiwa kuhusu kama Ikulu ya Urusi kama ilikubaliana na madai ya Rais wa Marekani Joe Biden kwamba huduma maalumu za Marekani zilikuwa na ufanisi zaidi kuliko za Urusi na pia kwamba Rais Vladimir Putin wa Urusi alikuwa na wasiwasi mkubwa juu ya hilo.

Akijibu swali hilo alis, Peskov alibainisha kuwa vikosi vya usalama vya Marekani vina nguvu na uwezo mkubwa.

“Hata hivyo, haisaidii mimi kusema ni nani mwenye nguvu na nani dhaifu. Kwa kawaida, itakuwa ajabu ikiwa mkuu wa serikali ya Marekani aliwaambia wafanyikazi wake wa usalama kitu tofauti, " alieleza.

Aliongeza, “Niamini tuna kila sababu ya kujivunia vikosi vyetu vya usalama."

Kiongozi wa Marekani aligusia suala la kazi ya huduma maalumu katika hotuba yake kwa uongozi na wafanyakazi wa usalama wa nchi hiyo Julai 27, mwaka huu.

 

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/651bd437a2eb69514d9e3bdf4d692302.jpg

Waziri wa Uingereza, Boris Johnson ametengua uteuzi wa ...

foto
Mwandishi: MOSCOW, Urusi

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi