loader
Dstv Habarileo  Mobile
Mzozo waibuka Somalia kuhoji masanduku ya UN

Mzozo waibuka Somalia kuhoji masanduku ya UN

MZOZO umeibuka nchini Somalia juu ya kwanini baadhi ya serikali zingine za majimbo zilipokea misaada ya masanduku ya kura kutoka Umoja wa Mataifa (UN).

Ofisi ya UN nchini Somalia (UNSOM) ilitoa vifaa vya uchaguzi kwa jimbo la Kusini-Magharibi, televisheni ya kitaifa ya Somali iliripoti.

Hata hivyo, baadhi ya watu mtandaoni wameitaja hatua hiyo kama tatizo la utegemezi, wakisema kwamba masanduku ya kura ambayo yametengenezwa kwa plastiki, yanaweza kununuliwa ndani ya nchi.

Wengine walisema ni aibu kwamba serikali haikuweza kufanya uchaguzi bila kupata misaada.

Majimbo ya Somalia yanatakiwa kufanya uchaguzi wa Bunge na Seneti ambao ulicheleweshwa juu ya mizozo kati ya wadau.

Majimbo hayo yako katika harakati za kuandaa uchaguzi wao wa seneti.

Jubbaland ilifanya uchaguzi wake jana.

Kucheleweshwa kwa uchaguzi siku za nyuma, kulisababisha vurugu kubwa katika mji mkuu Mogadishu wakati viongozi waliposhindwa kukubaliana jinsi uchaguzi utakavyofanyika.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/7e49a2e8e87d9f1d5be01ef6980927a8.jpg

Waziri wa Uingereza, Boris Johnson ametengua uteuzi wa ...

foto
Mwandishi: MOGADISHU, Somalia

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi