loader
Diamond azidi kukimbiza na Iyo

Diamond azidi kukimbiza na Iyo

NYOTA wa muziki wa kizazi kipya Nassibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ anazidi kukimbiza mtandaoni na video ya wimbo mpya wa Iyo alioshirikiana na wasanii wa Afrika Kusini.

Diamond ameimba wimbo huo na wasanii Lethabo Sebetso ‘Focalistic’, kundi la muziki la Mapara A Jazz na Ntosh Gazi.

Baada ya kuachia video hiyo ndani ya masaa mawili jana ilifikisha zaidi ya watazamaji laki mbili.

Msanii huyo kabla ya kuachia kazi yake hiyo tayari alitangaza ujio wake  kwenye mabango ya matangazo katika jiji la New York, Marekani na kupitia mitandao mbalimbali ya kimataifa hivyo, mapokezi yake yanaweza kuweka rekodi mpya.

Wimbo huo ambao ulitolewa katika mfumo wa sauti hivi karibuni ulifanya vizuri sehemu mbalimbali kutokana na aina ya uimbaji, mtindo na uchezaji wake unaofanana na ule unaotumika Afrika Kusini.

“Oyaa video ya Iyo ndio hiyo,”aliweka ujumbe huo kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram kuwajulisha mashabiki wake kazi mpya.

Diamond akiwa ni miongoni mwa wasanii wa Afrika wanaoongoza kwa kuwa na wafuasi wengi kwenye mitandao ya kijamii amekuwa akibadilika kwenye muziki wake akijaribu kutafuta soko kila kona ili kuwafikia mashabiki wengi wa ndani na nje ya nchi.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/cd787ae8db7ca11d1760d1ecbd4758c4.jpg

NCHINI Tanzania kuna matajiri wengi wakubwa walioanzia ngazi ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi