loader
Dstv Habarileo  Mobile
Solskjaer: Varane, Sancho watatubadilisha

Solskjaer: Varane, Sancho watatubadilisha

OLE Gunnar Solskjaer amesema, kuwasili kwa Jadon Sancho na Raphael Varane kumethibitisha nia ya Manchester United kufanya vizuri msimu mpya.

United imekubali kumsajili Sancho na Varane kwa ada ya pauni milioni 100 na Solskjaer amekiri huenda asihitaji tena zaidi wakati huu akijenga kikosi cha ushindani kwenye Ligi Kuu.

"Nina furaha tumefanya biashara na Real Madrid [usajili wa Varane]", Solskjaer alisema baada ya sare ya mabao 2-2 dhidi ya Brentford juzi usiku.

"Klabu imeonesha malengo yake kwa kusajili mmoja wa washambuliaji chipukizi duniani [Sancho] na mmoja wa mabeki wa kati wanaoheshimika duniani.”

"Kama nilivyosema mwanzo, kila kocha huwa na furaha anapokamilisha usajili mzuri, wachezaji hao wawili tuliowasajili wataleta tofauti kubwa.”

Kutokana na kusajiliwa kwa Varane, Solskjaer alisema Axel Tuanezbe, aliyekuwa akitakiwa Newcastle, anaweza kwenda kwa mkopo.

Phil Jones, ambaye hakucheza mechi za kimashindano kwa miezi 18 kutokana na kuwa majeruhi wa goti, anatarajiwa kuanza mazoezi mwishoni mwa wiki hii.

"Tukiwa na Raphael inaonekana kila kitu kinakwenda sawa, naona Axel anaweza kuondoka kwa sababu nina Raphael Varane, [Harry] Maguire, [Victor] Lindelof na Eric Bailly," alisema Solskjaer.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/4c76b71cb3aadf1225ba3b1fe49b2ba5.jpg

Ligi Kuu England leo inaendelea katika viwanja tofauti, ...

foto
Mwandishi: MANCHESTER, England

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi