loader
Dstv Habarileo  Mobile
Chelsea, Sevilla wazungumza juu ya  Kounde

Chelsea, Sevilla wazungumza juu ya  Kounde

CHELSEA na Sevilla zimeingia kwenye mazungumzo kuhusu kumsajili Jules Kounde Stamford Bridge msimu huu.

Vyanzo vinasema mchezaji huyo anaweza kusajiliwa kwa euro milioni 70.

Chelsea itamjumuisha na Kurt Zouma kwenye mpango huo, kwa mujibu wa vyanzo vya habari klabu hiyo ya Ligi Kuu tayari imeshatangaza thamani ya beki huyo wa Ufaransa.

Sevilla ilikubali mkataba wa aina hiyo na Tottenham Hotspur mapema wiki hii ambapo winga wa Hispania Bryan Gil alijiunga na Spurs kwa pauni milioni 25 na Erik Lamela akahamia upande wa pili.

Sevilla, iliyoilipa Bordeaux euro milioni 25 miaka miwili iliyopita na kumsajili beki huyo wa kati mwenye kipaji, ilikuwa na imani Manchester United ingeingia kwenye mbio za kumsajili Kounde, lakini klabu hiyo ya Old Trafford haikuweka ofa yoyote na badala yake kipaumbele chao ilikuwa kumsajili Raphael Varane.

Varane amekubali kujiunga United akitokea Real Madrid kwa uhamisho wa euro milioni 41 kama ilivyotangazwa rasmi Jumanne ya wiki hii.

Vyanzo vilisema, Madrid ilikuwa karibu ikimfuatilia Kounde kwa vile kocha wake wa zamani Zinedine Zidane alimkubali, lakini mpango huo ulikufa baada ya kiungo huyo wa zamani wa Ufaransa kuondoka klabuni hapo msimu uliopita.

Kounde, ambaye ana mkataba na Sevilla mpaka mwaka 2024, amecheza mechi 34 za ligi msimu uliopita na kuisaidia timu yake kufuzu Ligi ya Mabingwa.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 alikuwa sehemu ya kikosi cha Ufaransa kilichoshiriki Euro 2020 msimu huu na kucheza mechi moja waliyotoka sare ya mabao 2-2 na Ureno.

Hakucheza mechi ya kirafiki ya Jumanne ya wiki hii waliyotoka sare ya mabao 2-2 dhidi ya Paris Saint-Germain.

Kounde alikuwa kwenye benchi katika mechi ya tatu ya maandalizi ya msimu ya Sevilla na hakuzungumza na vyombo vya habari baada ya kuondoka uwanja wa Faro Algarbe.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/0dc8d5e6e947a63f4ffe6fd8259ca458.jpeg

WASICHANA waliopata ujauzito katika umri mdogo ...

foto
Mwandishi: LONDON, England

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi