loader
Dstv Habarileo  Mobile
TRA kufanya maboresho ulipaji kodi 

TRA kufanya maboresho ulipaji kodi 

 

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA), imewahakikishia walipakodi na wananchi wote kwa ujumla kuwa imejipanga vyema katika kuboresha usimamizi wa kodi nchini.

Hatua hizo ni kuboresha utoaji wa huduma zake, kupanua wigo wa elimu ya kodi, kuwezesha huduma mbalimbali kupatikana kwa njia ya kielekroniki, kuboresha mahusiano na walipakodi ikiwa ni pamoja na kuongeza kasi ya kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili.

Kamishna Mkuu wa Mamkala hiyo, Alphayo  Kidata alisema hayo Julai 30, 2021 katika taarifa  yake kwa Vyombo vya Habari ambayo iliyosomwa kwa niaba yake na Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi , Richard Kayombo katika Mamlaka hiyo mkoani Morogoro.

Kidata alisema jambo hilo litachangia kuongeza ari ya ulipaji kodi kwa hiyari na hivyo kuongeza makusanyo ya mapato ya Serikali yatakayoiwezesha kutoa huduma bora zaidi kwa wananchi pamoja na kutekeleza miradi ya maendeleo.

Alisema kuwa ili kupanua wigo wa kodi, Mamlaka ya Mapato Tanzania kuanzia mwezi Agosti 2021 itaendesha zoezi la kusajili wafanyabiashara wapya nchini kote kwa kuanzia na mkoa wa Dar es Salaam ili kuongeza ushiriki wao katika kuchangia mapato ya Serikali.

Hivyo alitoa wito kwa wafanyabiashara na wananchi wote kwa ujumla kujitokeza kwa wingi kushiriki katika zoezi hilo maalumu lenye lengo la kuhakikisha kila mfanyabiashara anachangia maendeleo ya nchi yetu badala ya kutegemea kundi dogo la walipakodi .

Pia alisema , zoezi hilo litaenda sambamba na kuhakiki matumizi sahihi ya Mashine za Risiti za Kielektroniki (EFD)  kwa wanyanyabiashara.

Kamishna Mkuu wa  Mamkala hiyo  pia aliwakumbusha wafanyabiashara wote kuzingatia wajibu wao wa kuwasilisha  ritani “return”  na kulipa kodi stahiki kwa wakati ili kuepuka riba na adhabu zisizo za lazima.

"Ofisi zetu za TRA nchi nzima ziko wazi kuwahudumia wananchi wote ikiwa ni pamoja na kutatua changamoto zozote zinazowakabili na kupokea mapendekezo ya kuboresha utendaji wetu wa kazi," alisema Kidata.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/fa55d7e8ddc2827666c7a631c9778d1b.jpg

WASICHANA waliopata ujauzito katika umri mdogo ...

foto
Mwandishi: John Nditi, Morogoro

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi