loader
Dstv Habarileo  Mobile
Tanesco haishikiki katika kuajiri wahandisi wanawake

Tanesco haishikiki katika kuajiri wahandisi wanawake

SHIRIKA la Umeme nchini (Tanesco), yaongeza kasi kuajiri wahandisi wengi wanawake tofauti na taasisi nyingine nchini.

Hilo lilibainika wakati wa kutolewa kwa tuzo mbalimbali katika maadhimisho ya siku ya wahandisi wanawake Tanzania yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Meneja Rasilimali Watu kutoka Tanesco, Francis Sangunaa akizungumza baada ya kupokea tuzo hiyo iliyotolewa na wahandisi wanawake alisema wanashukuru kwa kutambuliwa kama mwajiri bora wa kuajiri wanawake wengi zaidi katika sekta ya uhandisi.

Alisema sekta hiyo ni miongoni mwa sekta ambazo ushiriki wa wanawake upo katika kiwango cha chini lakini kwa shirika hilo limeweza kuajiri wale wenye sifa.

“Tunao wahandisi wanawake zaidi ya 76 na mafundi sanifu zaidi ya 98, na siri ya ushindi wao ni kwamba wale wanaoanza kazi wakiwa katika ngazi za chini,Tanesco hutoa nafasi ya kujiendeleza katika vyuo vyao vilivyopo maeneo mbalimbali kwenye mikoa ya Dar es Salaam, Arusha na Mbeya,” alisema.

Alisema pamoja na kuwa shirika hilo limeajiri wahandisi wanawake wengi, upatikanaji wao ni wa ushindani.

Naye Meneja Mradi wa SGR2 kutoka Idara ya Uwekezaji Kitengo cha Miradi Tanesco, Rosamystica Luteganya ambaye ndiye anayesimamia mradi wa reli toka Morogoro hadi Dodoma awamu ya pili alisema, “Siri ya mafanikio ya wanawake Tanesco kina mama wapo makini katika kulea familia hata wanapopewa kazi wanakuwa makini katika kazi zao hivyo siri kubwa ya mafanikio ni kujali kazi zao kufanya kwa weledi na kupenda kazi yao.

Kwa upande wake Katibu Msaidizi wa Jukwaa la Wanawake Wahandisi na Mafundi kutoka Tanesco, Catherine Shayo alisema siku hiyo ni ya muhimu kwao kwa ajili ya kuonyesha shughuli wanazofanya kuanzia umeme unavyozalishwa, unavyosafirishwa mpaka unavyosambazwa.

Kwa upande wake Mgeni Rasmi katika maadhimisho hayo Katibu Mkuu Kiongozi kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Zena Said alisema mpaka sasa takwimu zinaonyesha kuwa wahandisi wanawake bado wapo kidogo kama asilimia 11 tu ya wote walioko nchini.

Alisema kwa kutambua hilo kongamano kama hilo ni muhimu katika kuwahamasisha wanawake kusoma masomo ya sayansi ili idadi hiyo iweze kuongezeka.

 

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/6ae2e6222d547822696fcfad1949b06f.jpeg

WASICHANA waliopata ujauzito katika umri mdogo ...

foto
Mwandishi: Lucy Ngowi

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi