loader
Dstv Habarileo  Mobile
Profesa Sedoyeka: Anayefikiria upigaji apishe

Profesa Sedoyeka: Anayefikiria upigaji apishe

MKUU wa Chuo cha Uhasibu Arusha (AIA) Profesa Eliamani Sedoyeka amewataka wahasibu nchini kuhakikisha wanafanya kazi zao kwa kuzingatia maadili ya kazi ikiwa ni pamoja na kusimama katika weledi ili kuepuka malalamiko ya mara kwa mara ambayo yamekuwa yakiikumba kada hiyo.

Sedoyeka ameyasema hayo jana katika viwanja ya Mnazi kwenye maonyesho ya 16 ya vyuo vikuu na taasisi za elimu ya juu, kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Alisema ni vema wahasibu kote nchini kuhakikisha malipo yote yanayofanyika yapitie kwenye mfumo sahihi na kuachana na ujanja ujanja.

Amesema wamekuwa wakipokea malalamiko mengi kuhusu weledi wa wahasibu wanaowapeleka kwenye soko la ajira kitu ambacho hakipendezi.

“Tunapowapokea vyuoni tunawafundisha sheria za uhasibu na misingi ya kusimamia, kama mtu anafikiria kupiga uhasibu sio sehemu yake ataishia kufungwa, kila kitu kipo kwenye mfumo, unaweza kupiga ila  ujue ipo siku isiyo na jina utadakwa tu hata uwe mjanja vipi,” alisema na kuongeza

Alisema ili kuepuka vishawishi ni vema wahasibu wafutate utaratibu wa kutumia mifumo sahihi kitu ambacho anaamini kitasaidia kuondokana na changamoto ya malipo hewa pamoja na kukabiliana na tatizo kubwa la uingizwaji na uzagaaji wa fedha haramu.

Aidha akizungumzia wahitimu wengi wa vyuo vikuu wakidaiwa kushindwa kuonyesha umahiri kwenye sehemu za kazi, alisema AIA imejiwekea miongozo itakayowafanya wanafunzi kubobea kwenye fani wanazosoma kwa kuanzisha kozi za uanagenzi na pia  chuo kinashirikiana na waajiri kuwapa mafunzo wanafunzi wameweka pia miongozo inayomuelekeza mwalimu vitu vya kufundisha ili kumjengea ubobezi mwanafunzi.

Alisema katika chuo hicho wanajikita kumfundisha mtu kuwa mbobezi wa kozi husika na sio kuchukua shahada bila kuwa na umahiri.

Profesa Sedoyeka alisema kwenye maonyesho hayo wanatoa pia ushauri wa kozi kwa wanafunzi wanaotaka kujiunga na vyuo vikuu na taasisi za elimu ya juu.

Alisema, “Tunawashauri kozi gani zinawafaa kulingana na mtu na mapenzi yake, na chuoni kwetu tumeweka mazingira ambayo yatawafanya vijana kusoma, kufurahia ujana wakati wakitengenezwa kuwa wabobezi,”.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/e1f8b3eb5c6733cd7eeba280dbbe303e.jpg

WASICHANA waliopata ujauzito katika umri mdogo ...

foto
Mwandishi: Vicky Kimaro

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi