loader
Dstv Habarileo  Mobile
Zanzibar yahitaji dozi milioni moja za chanjo

Zanzibar yahitaji dozi milioni moja za chanjo

SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imesema inahitaji dozi milioni moja za chanjo dhidi ya ugonjwa wa Covid-19 ili kukidhi mahitaji ya wananchi wa Zanzibar.

Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Watoto, Nassor Ahmed Mazrui, alisema hayo wakati akipokea chanjo na kutoa shukrani kwa Serikali ya China kwa msaada wake wa chanjo 100,000.

Aliwataka wananchi kupuuza uvuvi kwamba chanjo hizo si nzuri kwa afya ya binadamu.

China imetoa chanjo aina ya Sinovic. Alisema chanjo inayotolewa na China kwa Zanzibar ipo salama na imethibitishwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) kwa ajili ya matumizi ya watu wote duniani.

Mazrui ambaye ni miongoni mwa viongozi wa kwanza kupata chanjo hiyo kwa upande wa Zanzibar, alisema tangu siku aliyopata chanjo zaidi ya wiki tatu sasa, yupo salama kiafya na hajapata matatizo yoyote kiafya.

“Napenda niwathibitishie wananchi kwamba, chanjo ya kujikinga na virusi vya corona ambayo mimi nimepatiwa ipo salama na tangu nilipochanjwa sijapata matatizo ya aina yoyote ya kiafya,”alisema.

Aidha, aliwataka wananchi wote nchini kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan baada ya kuwaongoza Watanzania kupata chanjo ya kujinga na Covid-19, Ikulu Dar es Salaam.

Chanjo iliyowasili juzi ni ya awamu ya pili ambayo ya kwanza ilitolewa ikiwa ni maombi ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa ajili ya mahujaji waliotarajiwa kufanya Ibada ya Hija Makka. Hata hivyo, hija hiyo iliahirishwa na Serikali ya Saudi Arabia.

Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Mnazimmoja, Dk Abdallah Suleiman, alisema mgao wa chanjo ya mwanzo ni kwa wafanyakazi wa sekta muhimu ikiwemo madaktari na wauguzi katika hospitali za serikali Unguja na Pemba.

Mapema Balozi Mdogo wa China aliyepo Zanzibar, Zhang Zhisheng, alisema nchi yake itaendelea kuisaidia Zanzibar katika sekta mbalimbali ikiwemo afya.

Alisema tayari chanjo ya Sinovic imegaiwa kwa watu bilioni 1.3 katika zaidi ya nchi 50 zinazoendelea ikiwa ni sehemu ya msaada huku nchi zilizofaidika na mgao huo zikipunguza kwa asilimia kubwa maambukizi ya ugonjwa Covid-19.

“Uhusiano wetu na Zanzibar ni mkubwa na wa kindugu…. Tumejikita katika sekta mbalimbali ikiwemo afya kwa kujenga Hospitali ya Rufaa ya Abdallah Mzee iliyopo Pemba,” alisema.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/a564c2b1e493bf6bcb1eee34d7364a74.jpg

WASICHANA waliopata ujauzito katika umri mdogo ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Zanzibar

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi