loader
Dstv Habarileo  Mobile
Yanga yalia na maandalizi

Yanga yalia na maandalizi

BAADA ya kulazimishwa sare na timu ya Nyasa Bullets kwenye mechi ya Kundi A ya ufunguzi ya michuano ya Kombe la Kagame, Kocha wa kikosi cha Yanga, Razak Siwa amesema kukosa muda wa maandalizi kumechangia washindwe kupata ushindi katika mchezo huo.

Katika mchezo huo, Yanga ilitumia wachezaji wengi wa kikosi cha vijana pamoja na wapya wawili ambao wamesajiliwa na timu hiyo kwa ajili ya msimu ujao.

Akizungumza mara baada ya mchezo huo kumalizika kwa sare ya bao 1-1, Siwa aliwapongeza wachezaji wake kwa kujitahidi kucheza vizuri ingawa walikuwa na muda mchache wa kufanya mazoezi pamoja, lakini aliahidi kupata ushindi katika mchezo wao wa pili dhidi ya Atlabara.

“Vijana wamejitahidi, unajua tulikuwa na siku tatu za mazoezi hapo hapo kuna wachezaji kama Dickson Ambundo na Jimmy Ukonde ni wageni kabisa kwenye timu wamekuja na kucheza kwahiyo tunayapokea haya matokeo na tunarudi kwenye uwanja wa mazoezi kurekebisha mapungufu yetu, naamini mechi inayokuja tutashinda,” alisema Siwa.

Kocha huyo alisema wakati wanaingia kwenye mchezo huo walijipanga kuhakikisha wanaanza michuano hiyo kwa ushindi, lakini imekuwa tofauti ingawa sare pia ni moja ya matokeo ya mchezo wa soka, hivyo kitu cha msingi kwao ni kuhakikisha wanavuka hatua hiyo na kucheza hatua inayofuata.

Aidha, kocha huyo aliwamwagia sifa wachezaji wapya, Ambundo na Julio, kuwa walicheza vizuri ingawa ugeni na uchovu wa safari viliwagharimu, lakini ana imani watafanya vizuri kwenye mechi zinazofuata.

Kwa upande wake, Kocha wa Nyasa Bullets, Kalisto Pasuwa alisema ameridhika na matokeo hayo, lakini akasema uchovu ndio sababu kubwa iliyochangia washindwe kuibuka na ushindi.

“Tumekubali matokeo ya sare 1-1 siyo mabaya kwetu kwasababu wachezaji wangu walicheza wakiwa na uchovu mkubwa kwani kabla ya kuanza safari tulicheza mechi ya ligi Ijumaa na Jumamosi tukawa safarini na tulipoteza muda mwingi pale kiwanja cha ndege kitu ambacho kiliwaongezea uchovu wachezaji hata mazoezi kujiandaa na mchezo hatukufanya, lakini siyo mbaya naamini tutafanya vizuri mechi ijayo,” alisema Pasuwa.

Kocha huyo alielezea kufurahishwa na mashindano hayo akisema yatasaidia kuzidi kukiimarisha kikosi chake kwa ajili ya kupigania ubingwa wa Ligi Kuu ya Malawi ambayo inajulikana kama TNM Super Leagu

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/bb090b9f4cead588dd3e15e4e8050139.jpg

NYOTA wa zamani wa Yanga, Charles Bonifasi Mkwasa ...

foto
Mwandishi: Mohamed Akida

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi