loader
Dstv Habarileo  Mobile
Samia ataka Tanzania itumie fursa Rwanda

Samia ataka Tanzania itumie fursa Rwanda

RAIS Samia Suluhu Hassan ameagiza Waziri wa Viwanda na Biashara, Profesa Kitila Mkumbo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Geoffrey Mwambe wakutane na wamiliki wa viwanda vitatu nchini Rwanda ili kutumia fursa zilizopo katika viwanda hivyo ikiwemo ya kuwauzia malighafi zinazopatikana nchini.

Taarifa ya Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Jaffar Haniu, ilieleza kuwa Rais Samia alitoa agizo hilo jana wakati akihitimisha ziara ya siku mbili nchini Rwanda kwa kutembelea viwanda kikiwemo cha kutengeneza simu za mkononi. Alipokuwa kwenye kiwanda hicho cha Mara Phone alijionea hatua mbalimbali za utengenezaji wa simu.

Taarifa hiyo kwa vyombo vya habari ilieleza kuwa, Rais Samia pia alitembelea kiwanda cha uunganishaji magari cha Volkswagen na kujionea hatua za kuunganisha vyombo hivyo vya usafiri vinavyouzwa nchini humo. Aidha, alitembelea kiwanda cha Inyange kinachotengeneza vinywaji.

Akiwa na mwenyeji wake Rais wa Rwanda, Paul Kagame, walijionea shughuli za uzalishaji wa bidhaa yakiwemo maji ya kunywa, maziwa na juisi.

Baada ya ziara hiyo Rais Samia aliagana na Rais Kagame katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kigali na kurudi Dar es Salaam.

Juzi Rais Samia alisema ziara yake ya siku mbili Rwanda ililenga kuimarisha na kukuza ushirikiano wa kiuchumi kati ya Tanzania na Rwanda.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/e91f8db8b9115a32c371416055052456.jpg

WASICHANA waliopata ujauzito katika umri mdogo ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi