loader
MATENDO YANAYOUDHI KATIKA MIRADI YA MAENDELEO MKOANI MARA

MATENDO YANAYOUDHI KATIKA MIRADI YA MAENDELEO MKOANI MARA

Miradi ya Maendeleo katika halmashauri za Serengeti, Tarime mjini, Tarime vijijini, Rorya, Bunda vijijini na Bunda mjini imekaguliwa na Mkuu wa Mkoa wa Mara, Ally Hapi na kubaini matendo tofauti yakiwemo yanayoudhi.

Matumizi ya milango ya vyuma kwenye vyumba vya madarasa na ofisi za walimu huku madirisha nayo yakiwa ya vyuma tena yasiyofunguka, yamepigwa marufuku na RC Hapi.

Amesema aina hiyo ya ujenzi huongeza hatari ikitokea ajali ya moto. 

Pia amesema majengo ya serikali hutakiwa kufuata viwango vinavyowekwa vyenye kuzingatia thamani ya fedha lakini yenye mwonekano unaovutia.

Machi Mwaka huu Serikali ilipeleka Sh bilioni Moja kuanza ujenzi wa  Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Bunda, kwenye Kijiji cha Kibara jimboni Mwibara.

Ilitakiwa ndani ya muda wa miezi sita mradi uwe umekamilishwa kwa kiwango cha fedha hiyo, lakini imekutwa hakuna tofali hata moja lililojengwa.

Mkandarasi bado anachimba msingi, hajaanza hata kukata nondo akisema tatizo hajapelekewa umeme.

Baadhi ya vifaa vikiwemo Nondo, Simenti na Miluda vilikutwa vimenunuliwa kwa mawakala, kinyume na maelekezo yanayotaka miradi mikubwa inunue vifaa kwa jumla, viwandani.

Matendo hayo yalisababisha utekelezaji wa mradi  huo kutiliwa shaka na RC na kuagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ichungeze nani aliuza vifaa hivyo na mazingira yote yanayozunguka manunuzi hayo.

Amesema ucheleweshwaji wa mradi huo una athari hasi kwa thamani ya fedha na inakwamisha malengo ya serikali ya kusogeza huduma jirani na wananchi.

Halmashauri hiyo pia inatekeleza mradi wenye thamani ya Sh bilioni 2.3 wa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya iliyopo Nyamuswa, ambapo ukaguzi uliofanywa na RC umebaini udanganyifu katika nyaraka za ununuzi(BOQ).

Kutokana na kasoro hizo na nyingine ameamua Afisa Manunuzi na Mhandisi wa Halmashauri hiyo wakamatwe na polisi kwa ajili ya kuhojiwa na TAKUKURU.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/65993ced875be3518ad64145f129ecd5.jpg

TAFITI mbalimbali zinaonesha kwamba uchafuzi wa mazingira ...

foto
Mwandishi: Editha Majura, Mara

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi