loader
Dstv Habarileo  Mobile
Rais Samia afanya uteuzi mpya, Othman Chande ndani

Rais Samia afanya uteuzi mpya, Othman Chande ndani

Rais Samia Suluhu, hii leo Agosti 17, 2021 amefanya uteuzi wa viongozi watakaoenda kushika nyadhifa za mbalimbali serikalini.

Rais Samia amemteua Jaji Mstaafu, Mohamed Chande Othman kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ardhi (ARU).

 

Pia, amemteua Prof esa Elisante Ole Gabriel kuwa Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania. Kabla ya uteuzi huu Profesa Ole Gabriel alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi  anayeshugulikia mifugo.

Ole Gabriel anachukua nafasi ya Mathias Kabunduguru ambaye amestaafu. Ole Gabriel ataapishwa Agosti 21, Ikulu jijini Dar es Salaam pamoja na mabalozi wateule watatu ambao ni;

Luteni Jenerali Yakub Hassan Mohamed ameteuliwa  kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uturuki, Mahmoud Thabit Kombo ameteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia na Elsie Sia Kanza ameteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Marekani.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/d381a6ce7ec15eb6561da21c20e0e983.jpeg

WASICHANA waliopata ujauzito katika umri mdogo ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi