loader
Dstv Habarileo  Mobile
Vyama 11 vyapinga shinikizo katiba mpya

Vyama 11 vyapinga shinikizo katiba mpya

MUUNGANO wa vyama 11 vya siasa visivyo na uwakilishi katika Bunge la Tanzania umesema havioni haja ya kuwapo shinikizo na kuanza upya mchakato wa katiba mpya.

Kwa mujibu wa vyama hivyo muda sahihi wa jambo hilo ukifika, watataka mchakato uanzie ilipoishia Rasimu ya Katiba Mpya iliyoandaliwa na Bunge Maalumu la Katiba, badala ya kuanza upya.

Vyama hivyo ni DP, NRA, NFP, Demokrasia Makini, UDP, ADC, ADA TADEA, SAU, Sauti ya Umma, TLP na CCK.

Vilibainisha hayo Dar es Salaam jana katika mkutano wa pamoja viliposisitiza kuwa, vinaunga mkono kauli ya Rais Samia Suluhu Hassan kwamba jambo hilo na mengine, yasubiri nchi ijenge uchumi kwanza.

“Sisi vyama 11 vya siasa visivyo na uwakilishi bungeni hatuungi mkono hoja ya kuanza mchakato mpya wa katiba, tunaunga mkono hoja ya Rais Samia ya kusubiri kwanza jambo hilo ajenge uchumi na hata kama tutahitaji katiba mpya, sisi tunataka ifufuliwe ile rasimu ya katiba ambayo iliishia hatua ya kutaka kupiga kura; iletwe tuipigie kura sasa,” alisema Katibu Mkuu wa DP, Abdul Mluya kwa niaba ya vyama vingine.

Mluya alidai kuwa serikali ilitumia fedha nyingi katika mchakato wa kwanza wa katiba mpya uliofikia hatua ya kupigiwa kura na ndipo baadhi ya wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba wakatoka nje kwa kususia.

“Sote ni wanasiasa tuna mitazamo tofauti ya siasa, lakini jambo la msingi ni lazima tuheshimiane. Sisi vyama 11 tunaona ni bora kama mchakato wa katiba utakapofikia muda wake kuanza, basi tumalizie ile rasimu ambayo ipo tayari na si kuanza upya kuleta gharama zisizo na tija ili hali upo ambao hatukuumalizia,” alisema.

Naye Katibu Mkuu wa Chama cha ADC, Doyo Hassan Doyo, alisema hawaungi mkono hoja ya kuanzisha upya mchakato wa katiba mpya. Alisema: “Rais (Samia Suluhu) kasema tumpe muda kwenye jambo hili la katiba ili ajenge kwanza uchumi ambao umetawanyika na Covid -19; Yeye ndiye mtawala na kiongozi wetu hatuwezi wote kuwa viongozi; tumempa awe rais kwa niaba yetu na ameangalia na kuona kwa hali halisi ya uchumi kwa sasa hawezi kuanzisha mchakato huo wa katiba na sisi tunaunga mkono.”

Aliwataka wananchi kuwa macho dhidi ya wanasiasa wanajaribu kujimilikisha mchakato wa katiba mpya kwa maslahi yao

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/49d7d9291edd271ccf445be3a7a183e4.jpg

WASICHANA waliopata ujauzito katika umri mdogo ...

foto
Mwandishi: Ikunda Erick

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi