loader
Dstv Habarileo  Mobile
TRA Kagera kukusanya bil 83/-

TRA Kagera kukusanya bil 83/-

MAMLAKA ya Mapato Tanzania Mkoa wa Kagera inategemea kukusanya shilingi bilioni 83 kwa mwaka wa fedha 2021/22.

Afisa msaidizi wa kodi ambaye anasimamia utoaji elimu na huduma kwa mlipa kodi mkoani hapa, Alex Mwambenja ametoa kauli hiyo wakati wa semina kwa wafanyabiashara wa Manispaa ya Bukoba Juu ya mabadiliko ya sheria na kanuni za kodi ili waweze kuyafanyika kazi.

Mwampenja amesema kuwa kiwango hicho wanategemea kukipata kutoka kwa wafanyabiashara na walipa kodi wengine hivyo wanapaswa kuwa tayari kulipa kodi kwa hiari ili kujenga uchumi wa nchi.

Ameongeza kuwa katika kuhakikisha TRA inapanua wigo wa kukusanya kodi, katika mwaka wa fedha 2020/21 wamesajiliwa walipa kodi wapya elfu 3,000 na mpaka sasa zoezi hilo linaendelea .

Nao baadhi ya wafanyabiashara waliopata semina Alice Katabarwa na Justuce Kandokola wameshauri mamlaka hiyo kufanya marekebisho katika mfumo wao wa kukusanya kodi kwa njia ya mtandao na kuhakikisha maafisa wa kodi wanafika katika eneo husika na kujiridhisha kabla ya kumkadiria mtu kiwango cha kodi ya mapato. 

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/0f8fb0103efa29d6c69bfa1116f89237.jpeg

WATANZANIA wametakiwa kuchangamkia fursa ...

foto
Mwandishi: Na Diana Deus, Bukoba

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi