loader
Dstv Habarileo  Mobile
Rais Samia aomba radhi akimwapisha Balozi wa Tanzania Marekani

Rais Samia aomba radhi akimwapisha Balozi wa Tanzania Marekani

Rais Samia Suluhu Hassan amemuomba radhi Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Elsie Sia Kanza kwa kumteua kwatika nafasi ya ubalozi bila kumshirikisha. 

Akiongea mapema leo baada ya kumuapisha, Rais Samia amesema "nimekutoa World Bank (Benki ya Dunia) na bila kukushauri."

Nimeona kazi nzuri unayofanya jinsi ulivyokwenda World Bank nikajua kwa nchi yetu ilivyofika sasa na nchi ya Marekani wewe ungetufaa kukaa pale. Kwanza nisamehe kwa kukutoa pale na nashukuru ndio uzalendo huo kwamba umekubali kurudi nyumbani kuja kutumikia nchi yako, amesema Rais Samia baada ya kumuapisha Balozi Mteule, Elsie Sia Kanza kuwa Balozi wa Tanzania nchini Marekani.

Rais Samia amekiri kwamba marekani bado ni taifa kubwa na lenye nguvu dunia. Kwa upande mwingine amesema Tanzania inaushirikiano mzuri na Marekani hususani ule wa Kisiasa na Kiuchumi. 

“Kwa msingi huo nakusihi sana balozi mpya ukahakikishe unakuza ushirikiano na uhusiano uliopo. Ubalozi wa Marekani unawakilisha pia nchini Mexico. Huna budi kuingia ingia huko nako hatujaanza nao mahusiano makubwa lakini si vibaya Tanzania ikajulikana huko pia,” amesema Rais Samia.

Mkuu huyo wa nchi amemtaka Balozi Kanza kuratibu vizuri shughuli za World Bank na IMF hasa upande wa fursa kwa kuwa ametoka huko.   

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/699375c1b220b4f3ea4e83a69f19c5f3.png

WASICHANA waliopata ujauzito katika umri mdogo ...

foto
Mwandishi: Na Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi