loader
Zifanye nywele zako kuwa na afya kwa vitu vya asili

Zifanye nywele zako kuwa na afya kwa vitu vya asili

NYWELE huwa zinapendeza zikitunzwa vizuri. Haijalishi ni nywele ndefu au fupi, umeweka dawa au hujaweka, lakini jambo la msingi ni kuhakikisha unazitunza vizuri.

Vile vile nywele nzuri ni zile zenye afya, zilizojaa vizuri ama ziwe hazina dawa au zenye dawa zote zinahitaji matunzo. 

Katika safu yetu leo tutaangalia namna ya kutunza nywele na kuzifanya kuwa nzito, zilizojaa na afya kwa kutumia vitu vya asili kabisa. Dondoo zifuatazo zitakusaidia kuzifanya nywele zako kujaa

Mafuta ya kastoroli na kitunguu

Maji ya vitunguu huzalisha aina ya protini inayojulikana kitaalamu kama collagen na husaidia nywele kukua. Mafuta ya kastoroli huchochea ukuaji wa nywele na kuimarisha vinyweleo.

Weka katika bakuli mafuta ya kastori na maji ya kitunguu. Changanya vizuri, kisha paka katika ngozi ya kichwa kwa kutumia pamba.

Mafuta ya nazi na amla

Mafuta ya nazi ni tiba nzuri kama unataka nywele zako ziwe ndefu na kung’aa. Amla hufanya mizizi ya nywele kuwa na nguvu.

Katika bakuli weka mafuta ya nazi pamoja na unga wa matunda ya amla. Changanya vizuri, halafu paka kwenye ngozi ya kichwa kwa kutumia pamba.

Tui la nazi na uwatu (fenugreek)

Tui la nazi lina mafuta ya asili yenye asidi inayofanya nywele kuwa na hali ya unyevunyevu. Hivyo inasaidia kurejesha afya ya nywele na ngozi na hufanya kazi kubwa kama conditioner kwa nywele zilizoharibika.

Mbegu za uwatu ni chanzo kikubwa cha chuma na protini, vitu viwili muhimu katika kukuza nywele.

Changanya tui la nazi na unga wa mbegu za uwatu na kutengeneza uji mzito. Paka mchanganyiko huo taratibu kwenye ngozi ya kichwa na acha kwa dakika 30. Kisha osha nywele zako kwa shampuu na malizia kwa kupaka conditioner. Fanya mara moja au mara mbili. 

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/c195773e2597861bb0b2076f157213c7.jpg

NCHINI Tanzania kuna matajiri wengi wakubwa walioanzia ngazi ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi