loader
Dstv Habarileo  Mobile
Samia ataka michezo isimamiwe vizuri

Samia ataka michezo isimamiwe vizuri

RAIS Samia Suluhu Hassan ametaka michezo isimamiwe vizuri. Hayo aliyasema jana Ikulu, Dar es Salaam alipokutana na wanamichezo, wakiwemo wale wa timu ya taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 23.

Timu ya taifa ya U-23 ilitwaa taji la Michuano ya Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati ya `Cecafa Challenge Cup 2021’ Julai 30 mwaka huu nchini Ethiopia na jana ililikabidhi taji hilo kwa Rais Samia.

Rais ameitaka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Shirikisho na Vyama vya Michezo, klabu pamoja na wanamichezo wenyewe, kujipanga vizuri ili kuleta matokeo mazuri katika mashindano mbalimbali ya kimataifa.

Alisema ni aibu kuona taifa lenye watu zaidi ya milioni 50 kuwakilishwa na wanamichezo watatu kwenye Michezo ya Olmpiki na kumwagiza Kaimu Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo, Neema Msitha kuhakikisha michezo inasimamiwa ipasavyo ili kupata wawakilishi wengi katika michezo ya kimataifa.

Pia aliwataka viongozi wa michezo kuwapa moyo wachezaji wanapofanya vibaya kuliko kuwatusi na kawashambulia, lakini ni vyema wakawapa moyo ili wafanye vizuri zaidi, wawalee wachezaji kwa mapenzi.

Ametaka kuangaliwa vyema kwa wanamichezo nchini ili wanapostaafu au kuumia, wawe na maisha bora tofauti na hali ilivyo sasa, ambapo wengi wao wamekuwa na maisha duni yasiyo akisi mchango wao kwa Taifa.

Halikadhalika, amewataka viongozi wa klabu, vyama na mashirikisho ya michezo nchini kuzingatia masuala ya utawala bora kwa kuhakikisha wanafuata Katiba, Sheria na taratibu za taasisi zao kwa kudhibiti vitendo vya wizi, ubadhirifu, upendeleo na upangaji matokeo, ambavyo vinakwamisha ukuaji na ustawi wa sekta ya michezo nchini Alisema amefurahia kupokea kombe na hiyo ni mara ya pili akipokea kombe kwa timu za soka, hivyo anaamini kila safari huanza na hatua moja, na ni safari ya kwenda kuchukua makombe mengine makubwa mbele ikiwa tu vijana watatunzwa.

“Nawapongeza vijana wetu wa U-23, ni imani yangu ushindi wenu kwenye Cecafa utawahamasisha vijana wengine kufanya vizuri,

Taifa Stars inajiandaa na michezo ya kufuzu Kombe la Dunia2022 Qatar, Twiga Stars pia wanajiandaa na Cosafa ni imani yangu watajiandaa ili wakashinde,” alisema Samia.

Pia aliwakumbusha wanamichezo kwenda kuchanja, hasa wale ambao hawajachanja kwani kila wanaposafiri vipimo vya corona vinawasubiri.

Awali, Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa alisema wanawake katika michezo mbalimbali ndio wanaongoza kufanya vizuri na mwaka huu wameanzisha Tanzanite Women Sportsfestival.

Miongoni mwa wanamichezo waliopongezwa ni timu ya U-23 na benchi la ufundi na wanariadha watatu walioshiriki Michezo ya Olmpiki Tokyo 2020 mwaka huu, Alphonce Simbu aliyemaliza wa saba, Failuna Abdi nafasi ya 24 na Gabriel Geay, ambaye hakumaliza

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/f57eaf9084b83e8db49a7fb538bd09e4.jpg

KOCHA Mkuu wa Kagera Sugar, Francis ...

foto
Mwandishi: RAHEL PALLANGYO

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi