loader
Dstv Habarileo  Mobile
Samia aibeba ligi ya wanawake Cecafa

Samia aibeba ligi ya wanawake Cecafa

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amekubali kudhamini mashindano ya Ligi ya Mabingwa ya Wanawake Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) yatakayofanyika nchini Kenya kuanzia Agosti 28.

Rais Samia aliyasema hayo Dar es Salaam jana katika hafla ya kupokea Kombe la Michuano ya Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati ya Kombe la Cecafa Chalenji 2021, katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam na kuwapongeza wachezaji wa timu ya U-23 na wanariadha walioshiriki mashindano ya Olimpiki Tokyo 2020.

Samia alisema Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia ambaye pia ni Rais wa Cecafa ndiye aliyemshawishi na kumwomba aige kile anachofanya Rais wa Rwanda, Paul Kagame ambaye anadhamini Cecafa ya wanaume na akaomba bajeti ya mashindano hayo akaona anaweza, akakubali.

“Kuna ombi nilinong’ona na Rais wa TFF, aliniambia anataka kuanzisha mash-indano ya Cecafa Women Championship na yanataka udhamini, akanishawishi kwa kusema mwenzako Kagame anadhamini mashindano fulani na wewe dhamini haya.

Alisema kuna haja ya kuwatazama wachezaji wanawake hasa wa mpira wa miguu, kwani na wao wana maisha baada ya mpira siyo kuwashangilia kipindi wakileta makombe lakini mwisho wao maisha yao yanakuwa mabaya.

“Wachezaji wanawake wanatufurahisha wanavyoleta makombe ila wakiwa hawana afya ya kucheza watakuwa na maisha gani?, Tujiulize tumewaandalia nini!, wengi hawana ndoa na kwa walivyo ndoa kwao ni ndoto, ukimchukua kumpeleka nyumbani, mama atauliza huyu mwanamke au mwanaume?” alisema Samia.

Pia alimtaka Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa kuwatazama wachezaji wanawake, hasa mpira wa miguu pale watakapoanzisha tamasha la michezo la wanawake ‘Tanzanite Women Sportsfestival’ .

Alisema serikali imezingatia na imedhamiria kukuza michezo nchini kwa sababu inatangaza nchi na wameanzisha Mfuko wa Maendeleo ya Michezo, ambao una Sh bilioni 1.5 na kusema utaendelea kutunishwa.

Awali, akizungumza Rais wa TFF, Karia alimpongeza Rais Samia kwa kuhudhuria mpira wa miguu wa Ligi Kuu uliozikutanisha Simba na Yanga, kutoa punguzo kwa nyasi bandia na kuruhusu wawekezaji katika sekta michezo.

Alisema katika kipindi cha uongozi wake, TFF wamepokea mataji 10, manne yakiwa ni ya timu za wanawake, ambazo Rais Samia alikuwa mlezi wao.

Mashindano ya Cecafa ya klabu ni mashindano mapya, ambayo yatachezwa katika makundi mawili yenye timu nne kila moja.

Mwakilishi wa Tanzania, Simba Queens ya Tanzania Bara na New Generation kutoka Zanzibar timu nyingine zinazoshiriki ni PVP Buyenzi mabingwa wa Burundi na Lady Doves, ambao ni mabingwa wa Uganda, FAD FC, Yei Joint Stars FC, Vihiga Queens na Comercial Bank of Ethiopia FC.

Bingwa wa Cecafa ataungana na mabingwa wengine katika kanda nyingine za Caf katika fainali zitakazofanyika Misri pamoja na timu mwenyeji Misri na timu inayoshikilia kombe.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/f2076435ff7cf22fc293d0e11bafe961.jpg

KOCHA Mkuu wa Kagera Sugar, Francis ...

foto
Mwandishi: RAHEL PALLANGYO

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi