loader
Dstv Habarileo  Mobile
Manara rasmi Yanga

Manara rasmi Yanga

KLABU ya Yanga imemtambulisha aliyekuwa msemaji wa Simba Haji Manara kuwa msemaji wake mkuu.

Hafla hiyo imefanyika jana kwenye ukumbi wa Serena Hoteli jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa utambulisho huo Manara aliushukuru uongozi wa Yanga kwa kumpa nafasi hiyo na yeye atatumia uzoefu wake wote kuifanya timu hiyo izidi kuwa kubwa Afrika.

“Nichukue fursa hii kuushukuru uongozi wa Yanga kwa kunipa nafasi hii maana wangeweza ku- kataa kutokana na namna nilivyokuwa nikiwasema wakati nipo Simba lakini yote ilikuwa ni sehemu ya kazi”.

Manara alisema kilichomshawishi kukubali kufanya kazi Yanga ni malengo waliyokuwa nayo klabu hiyo kuelekea msimu ujao na atahakikisha timu yake mpya inabeba taji la 28 la ligi kuu ya Tanzania Bara.

Alisema kingine kili- chomshawishi ni usajili bora uliofanywa na Yanga kuelekea msimu huu akisisitiza Wanayanga sio
tena muda wa kulalamikia waamuzi na Shirikisho la Soka Tanzania kwani usajili wa msimu huu unajitosheleza kutwaa ubingwa Aidha, Manara ambaye ukoo wake ni zao la Yanga amewaomba mashabiki wa Simba wasimchukulie vibaya kwani hana tabu na klabu, bali viongozi wake waliomuumiza vya kutosha.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/8c72a90acbb80169ee84628c84108fd6.jpg

KOCHA Mkuu wa Kagera Sugar, Francis ...

foto
Mwandishi: Na Mohamed Akida

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi