loader
Dstv Habarileo  Mobile
Simba yawatoa wawili kwa mkopo

Simba yawatoa wawili kwa mkopo

Mabingwa wa soka Tanzania bara Simba wamethibitisha kuwatoa kwa mkopo kwenda timu mbili tofauti nyota wake wawili, David kameta 'Duchu' na Ibrahimu Ame.

Kwa mujibu wa akaunti ya Twitter ya klabu hiyo Duchu ameelekea Biashara United Mara na Ibrahimu Ame amejiunga na Mtibwa Sugar ya Morogoro.

“Miongoni mwa wachezaji walioondoka kambini Morocco ni Ibrahimu Ame na David kameta Duchu ambao wametolewa kwa mkopo”, imesema taarifa ya Simba.

Mabeki hao walijiunga na Simba mwanzoni mwa msimu uliopita huku Ame akitokea Coastal Union ya Tanga kama mlinzi wa kati wakati Duchu akitokea Lipuli ya Iringa kama mlinzi wa pembeni.

Wote wawili wamekuwa hawapati nafasi za mara kwa mara katika kikosi cha kwanza cha klabu hiyo ya Msimbazi.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/98783d51dbe124109d3ff95ee0a89d07.jpeg

NYOTA wa zamani wa Yanga, Charles Bonifasi Mkwasa ...

foto
Mwandishi: Robinson shoo

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi