loader
Dstv Habarileo  Mobile
Ni Wananchi leo

Ni Wananchi leo

YANGA mpya itakayoshiriki Ligi Kuu na Michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika leo itashuka dimba la Benjamin Mkapa kucheza na Zanaco FC ya Zambia ukiwa ni mchezo wa kirafiki, ambao ni maalumu kwa ajili ya kuhitimisha kilele cha Tamasha la Wananchi, ambalo lilizinduliwa Zanzibar mapema wiki hii.

Tamasha hilo linalofanyika kwa msimu wa tatu mfululizo, lengo lake kuu ni kutambulisha kikosi cha wachezaji na benchi la ufundi kitakachoshiriki michuano msimu ujao, timu ya vijana chini ya umri wa miaka 20, timu ya Wanawake inayoshiriki Ligi Kuu, na jezi mpya ambazo zitatumika kwa msimu huo.

Mashabiki wengi wa Yanga, wanatarajiwa kujazana uwanjani kushuhudia usajili mpya uliofanywa hivi karibuni na uongozi wao ambao umekuwa na utofauti mkubwa na sajili zilizopita kitu ambacho kinawapa shauku ya kutaka kuwashuhudia nyota hao wakikabiliana na Zanaco ambayo ni moja ya timu kigogo nchini Zambia.

Baadhi ya nyota wapya walisajiliwa na Yanga kwenye dirisha kubwa ni pamoja na kipa wa timu ya taifa ya Mali Dijigui Diarra, mabeki Yannick Litombo, Djuma Shaban na washambuliaji Jesus Moloko, Fiston Mayele na Heritier Makambo bila kumsahau kiungo kutoka Uganda Khalid Aucho.

Mbali na nyota hao wa kimataifa, pia Yanga imesajili wachezaji kadhaa wazawa, ambao ni kipa Erick Johora aliyekuwa akiidakia Eagle Noir ya Burundi, pia yupo David Brayson anayecheza beki wa kushoto kutoka KMC, Yusuph Athuman anayecheza nafasi ya ushambuliaji kutoka Biashara United na winga Dickson Ambundo kutoka Dodoma Jiji.

Maingizo hayo mapya yameungana na nyota wengine 14 waliokua wanaunda kikosi cha Yanga cha msimu uliopita, ambapo sasa wamekutana na mtaalamu wa mbinu Nasriddine kabla ya kuanza kuonesha kile ambacho mashabiki wengi wa Yanga wanakitarajia kukiona kuanzia leo dhidi ya Zanaco pale kwa Mkapa.

Mashabiki wengi wa Yanga, wamekuwa na matumaini makubwa kwamba timu yao msimu ujao itavunja ufalme wa watani zao Simba na kurudi kwenye utawala, hiyo yote ni kutokana na usajili ambao umefanywa kupitia dirisha hilo la usajili, ambalo wanaamini wana kikosi bora kuzidi mabingwa watetezi Simba.

Mchezo huo pia ndio hutoa taswila halisi kwa mashabiki kwamba timu yao inaweza kumaliza ufalme wa Simba, ambao nao msimu huu hawatakuwa na nyota wao wawili muhimu kwenye kikosi chao, ambao ni Luis Miquissone na Cletus Chama.

Pia kutakuwa na burudani nyingine nyingi, ikiwemo ile ya muziki ambayo itaongozwa na nguli wa muziki wa dansi Koffi Olomide ambaye anatarajia kupamba tamasha hilo akishirikiana na wasanii 16 wa Tanzania.

Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli alisema maandalizi yote yamekamilika na uwanja huo unatarajiwa kufunguliwa mapema kuanzia majira ya saa 3:00 asubuhi na kutakuwa na kila kitu, kiwemo vyakula na michezo tofauti lengo likiwa ni kuwapa burudani mashabiki wao.

Zanaco ambayo iliitoa Yanga kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa misimu mitatu iliyopita, tayari iko nchini na kikosi chao kamili kwa ajili ya kuwakabili wenyeji wao.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/0b80b72dd5643b6ce96d7d2627c4b750.jpg

KOCHA Mkuu wa Kagera Sugar, Francis ...

foto
Mwandishi: Mohamed Akida

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi