loader
Dstv Habarileo  Mobile
Gomes yamemkuta Caf

Gomes yamemkuta Caf

WAWAKILISHI wa Tanzania katika michuano ya Ligi ya Mabingwa wa Afrika, Simba watawakosa makocha wake katika mechi hizo za kimataifa baada ya kutokuwa na leseni A ya Caf au Uefa Pro.

Kwa mujibu wa Shirikisho la Soka Afrika, Caf, kocha wa Simba, Didier Gomes ni miongoni mwa makocha waliotajwa kutokuwa na sifa hizo, akiwa na Leseni ya Uefa A Diploma wakati Caf wanataka Leseni A au Uefa Pro kwa kocha mkuu.

Wakati kocha Gomes akikaa jukwaani pia msaidizi wake, Seleman Matola mwenye leseni C ya CAF na sasa anaendelea na kozi ya leseni B, naye atakaa jukwaani kwa mechi za mwanzo kwa sababu hajamaliza masomo ya Leseni B ya Caf, ambayo inatakiwa kuwa nayo kwa kocha msaidizi.

Kaimu Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga alisema wamejiandaa kwa hilo kwa sababu walishafahamu suala hilo mapema.

“Leseni ya Uefa A na Caf A zote zilikuwa na kiwango kimoja wala haikuwa na shida, mwaka huu ndio wamekuja na hili la kulinganisha leseni ya Caf A na Uefa Pro tofauti na Uefa, A ambayo Gomes anayo,”.

“Lakini Didier yupo kwenye masomo ya Leseni A Uefa Pro kwa masomo ya online (mtandaoni) na atahitimu kabla ya raundi ya pili ya michuano ya Caf, hiyo kozi ni ya siku 15-27 tu,” alisema Kamwaga.

Kwa mujibu wa Simba ni kati ya timu timu 10 ambazo hazitaanza hatua ya awali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika pamoja na Wydad Casablanca, Raja Casablanca, Zamelek, Al Ahly, Es Tunis, Esente Setif, Horoya, Mamelod na TP Mazembe.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/f74b5b11283a7b60388bf1c4defce9d0.jpeg

NYOTA wa zamani wa Yanga, Charles Bonifasi Mkwasa ...

foto
Mwandishi: Rahel Pallangyo

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi