loader
Dstv Habarileo  Mobile
MAJALIWA ASIFU MICHEZO, BURUDANI

MAJALIWA ASIFU MICHEZO, BURUDANI

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa, amesifu maendeleo ya michezo nchini kutokana na mwamko mkubwa wa masuala ya sanaa, burudani na michezo.

Waziri Mkuu alitoa pongezi hizo jana alipoahirisha Bunge Jijjni Dodoma ambapo alisema, michezo imekuwa chanzo kikubwa cha biashara, utalii, kuimarisha afya na ajira kwa vijana wetu.

“Serikali imeendelea kuchukua hatua za makusudi za kukuza michezo nchini. Hatua hizo zinahusisha kuundwa kwa Mfuko wa Maendeleo ya Michezo na kurejesha mashindano ya UMITASHUMTA, UMISSETA na SHIMIWI,” alisema.

Waziri Mkuu alimpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia kuanzishwa kwa mfuko wa Maendeleo ya Michezo nchini na kukubali kudhamini mashindano ya wanawake ya Baraza la vyama vya Soka kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati (Cecafa).

Katika mashindano hayo yaliyomalizika juzi, Rais Samia alitoa udhamini wa dola za Marekani 100,000 (zaidi ya Sh milioni 230,000) ambapo sasa mashindano hayo yatajulikana kama Samia Cup.

Waziri Mkuu alisema, mfuko wa Maendeleo ya Michezo, utasaidia upatikanaji wa fedha kwa ajili ya kuziandaa vyema timu za Taifa za michezo mbalimbali na kuziwezesha kushiriki kwa tija katika mashindano na michezo ya kimataifa.

“Kama nilivyotangulia kueleza, michezo ni biashara na imekuwa chanzo muhimu cha ajira hususan kwa vijana,” alisema.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/4925d2031f733d666f1b0b90f303bef8.jpeg

NYOTA wa zamani wa Yanga, Charles Bonifasi Mkwasa ...

foto
Mwandishi: Magnus Mahenge, Dodoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi