loader
Serikali yarejesha magari 20 yaliyoibwa Kenya

Serikali yarejesha magari 20 yaliyoibwa Kenya

MKUU wa Wilaya ya Loitokitok nchini Kenya, Wesley Koech ameishukuru na kuipongeza serikali ya Tanzania kufanikisha kukamata na kurejesha magari 20 na pikipiki zilizoibwa nchini humo.

Koech alisema hayo jana mjini Loitokitok, Kenya katika kikao cha ujirani mwema kati ya wilaya hiyo na wilaya ya Rombo, Tanzania. Koech alisema serikali ya Kenya imeimarisha uhusiano wa ujirani mwema na Tanzania na wataimarisha uhusiano na wananchi wa Rombo.

Mkuu wa Wilaya ya Taveta, nchini Kenya, Joseph Maina alisema Tanzania inastahili pongezi kwa kuwasamehe na kuwachia huru maofisa polisi wa Kenya walioingia nchini wakiwa wamebeba silaha za moto. Mkuu wa Wilaya ya Rombo, Hamisi Maigwa alisema serikali ya Tanzania imejipanga kuondoa kero na vikwazo vinavyoathiri ujirani mwema kati ya Rombo na Loitokitok.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/6f5e4170bbaa7b69d42244bac6233402.jpeg

RAIA wa Kenya wamepiga kura kwa amani na ...

foto
Mwandishi: Na Upendo Mosha, Loitokitok

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi