loader
Dstv Habarileo  Mobile
Kamati ya Bunge yafundishwa diplomasia ya uchumi

Kamati ya Bunge yafundishwa diplomasia ya uchumi

WAJUMBE wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) wanakutana Dar es Salaam kufundishwa masuala kadhaa ikiwamo itifaki na dilpomasia ya uchumi.

Kamati hiyo pia itajifunza mawasiliano ya kidiplomasia na usalama wa kimtandao ili kujiimarisha katika kutekeleza majukumu yao. Mafunzo hayo ya siku tano yaliyoanza jana, yameandaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa kushirikiana na Chuo cha Diplomasia.

Wakati akiyafungua mafunzo hayo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula alisema kamati hiyo itapata ujuzi kuhusu mambo yenye maslahi kwa nchi. Alisema wizara hiyo ina amini kuwa wajumbe wa kamati na washiriki wengine watautumia ujuzi watakaoupata kuishauri wizara ndani na nje ya Bunge katika kulinda taswira ya Tanzania.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/59e9e61a038058f0f850ff288fbfc4d3.jpeg

WASICHANA waliopata ujauzito katika umri mdogo ...

foto
Mwandishi: Na Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi