loader
Dstv Habarileo  Mobile
ALAT yataka viongozi wenye weledi

ALAT yataka viongozi wenye weledi

JUMUIYA ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) inatarajia kufanya uchaguzi wake mkuu Septemba 27 hadi 29, mwaka huu huku wajumbe wakitakiwa kuchagua viongozi wenye weledi kwa manufaa ya taifa.

Akizungumza jana jijini hapa Katibu Mkuu wa ALAT, Elirehema Kaaya, alisema uchaguzi huo utafanyika Dodoma huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Rais Samia Suluhu Hassan. Alitaja nafasi zinazowaniwa ni ya Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na wajumbe 16 wa kamati tendaji ya jumuiya hiyo. “Awali, mkutano maalumu wa uchaguzi ulipaswa ufanyike Aprili (mwaka huu) lakini kutokana na taifa kuwa kwenye maombolezo umesogezwa mpaka mwezi huu,”alisema.

Alisema wanachama ambao wanagombea kwa nafasi ya mwenyekiti na makamu wanatakiwa kuhakikisha wanapata udhamini wa watu 10 ikiwa ni wawili wa kisasa na watendaji kutoka kwenye kanda tano za jumuiya hiyo. “Kwa upande wa watia nia kwenye nafasi ya ujumbe wa kamati tendaji wanapaswa kupata wadhamini wawili kutoka kundi la kisasa na watendaji katika kanda husika,”alisema.

Nafasi za wajumbe wa Kamati Tendaji zinazowaniwa ni nafasi tano za wagombea kutoka mamlaka za halmashauri za majiji, manispaa na miji, nafasi tano za wawakilishi kutoka halmashauri za wilaya. Pia wakurugenzi wawili kutoka halmashauri za majiji, miji na manispaa, wakurugenzi wawili wa halmashauri za wilaya na wawakilishi wawili wa wabunge. Kanda za ALAT ni Pwani, Kaskazini, Kati, Nyasa za Juu Kusini na Kusini.

Alisema wagombea wanapaswa kuhakikisha fomu zao zinafika Ofisi ya Katibu Mkuu kabla ya Septemba 26, mwaka huu. Akizungumzia wajumbe wa mkutano huo maalumu, Kaaya alisema ni kutoka mameya na wenyeviti wa halmashauri za majiji, manispaa, miji, na halmashauri za wilaya na wakurugenzi watendaji wa halmashauri za majiji, miji, manispaa na halmashauri za wilaya.

Alisema wajumbe wengine ni wawakilishi wa wabunge kutoka kwenye mikoa 26 na makatibu tawala wa mikoa wasaidizi. Madiwani wa Jiji la Dodoma wamealikwa kushiriki. Aidha, alisema baada ya kukamilika kwa uchaguzi watatumia siku mbili nyingine kuhakikisha wajumbe wa mkutano wanapitishwa kwenye mada mbalimbali za kuwajengea uwezo.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/0bdf51151bfd45b55d7b5ee276cce859.jpeg

WASICHANA waliopata ujauzito katika umri mdogo ...

foto
Mwandishi: Na Anastazia Anyimike, Dodoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi