loader
Dstv Habarileo  Mobile
UEFA yarejea ni vita ya Barca na Bayern

UEFA yarejea ni vita ya Barca na Bayern

Ligi ya Mabingwa barani Ulaya leo inarejea rasmi kwa michezo kadhaa kupigwa kwenye madimba tofauti huku mchezo mkubwa unaotazamiwa na watu wengi ukiwa Barcelona dhidi ya Bayern Munchen.

Timu mbili kutoka England, Chelsea watakuwa nyumbani kuwakaribisha Zenit na Manchester United itakuwa Switerzland kuvaana na Young Boys, mchezo wa mapema utakochezwa saa 1:45 usiku, mchezo mwingine wa muda huo, ni kati ya Sevila na Salzburg.

Juventus itakuwa Sweden kukipiga na Malmo ya nchini humo, Villareal itakuwa nyumbani dhidi ya Atalanta, Lille pia itakuwa nyumbani dhidi ya Wolfsburg, Dynamo Kyiv watakuwa nyumbani dhidi ya Benfica.

Michezo mingine itaendelea kesho ambapo, Inter Milan watakuwa San Siro kuwakaribisha Real Madrid, Liverpool dhidi ya AC Milan, Manchester City watavaana na RB Leipzig, Atletico Madrid na FC Porto.

Paris itakuwa ugenini kuvaana na Club Brugge KV, na Besiktas itaikaribisha Dortmund, Sherriff Tiraspol na Shakhtar Donetsk na mchezo wa mwisho utakuwa ni kati ya Sporting CP dhidi ya Ajax.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/b6b5c8279ead2d91f3197e12e4fc1b06.jpg

Kiungo mshambuliaji wa Brazil, Neymar JR amesema Kombe ...

foto
Mwandishi: Na Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi