loader
Dstv Habarileo  Mobile
Usione ‘Soo’, Jipange Uhesabiwe

Usione ‘Soo’, Jipange Uhesabiwe

KAMISAA wa sensa ya watu na makazi, Anne Makinda, amewataka watanzania kujitokeza kwa fahari  na kujipanga kuhesabiwa kwani kutofanya hivyo ni aibu kubwa.

Makinda ameyasema hayo leo uwanja wa Jamhuri Dodoma katika uzinduzi wa Mkakati wa Uelimishaji na Uhamasishaji wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 yenye kauli mbiu ‘Sensa kwa Maendeleo, Jiandae Kuhesabiwa’.

“Ni aibu kutokuhesabiwa 2022, jitokezeni kwa ufahari mkubwa, msikubali kupitwa, Sensa ni muhimu kwa mustakabali wa maisha yako,” alisema Makinda ambaye pia ni Spika wa Bunge mstaafu.

Amesema sensa ya sasa itakuwa shirikishi na itaanzia ngazi ya vitongoji hivyo viongozi wa vitongoji vyote lazima watambue umuhimu wa zoezi hilo.

Ametoa wito kwamba siku ya kuhesabiwa itakapofika kila mtu akimbilie kuhesabiwa.

“Sensa itatufanya tujulikane tuko wangapi…kweli mwenyekiti wa kitongoji utashindwa kuwajua watu wako?

“Vitongoji wote tukihesabu watanzania wote watakuwa wamehesabiwa, mtanzania mwenzangu jitokeze uone fahari kuhesabiwa, ukiwa hukuhesabiwa usimwambie mtu maana ni aibu,” alisisitiza.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/09f7fb2e54bc73616e516f058598b350.JPG

WASICHANA waliopata ujauzito katika umri mdogo ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi