loader
Dstv Habarileo  Mobile
Rais Samia azindua mkakati, uelimishaji, uhamasishaji wa sense

Rais Samia azindua mkakati, uelimishaji, uhamasishaji wa sense

Rais Samia Suluhu leo amezindua Mkakati wa Uelimishaji na Uhamasishaji wa Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 , uzinduzi uliofanyika mjini Dodoma.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Rais Samia alisema kuwa sensa hiyo itasaidia kujua maendeleo yaliyopatikana tangu ilipofanyika sensa ya mwisho ya mwaka 2012. 

Alisema zoezi hilo litasaidia Serikali kuandaa sera na mipango mipya ya maendeleo ya muda mfupi na muda mrefu na jinsi ya kuitekeleza na kufatilia utekelezaji wa mipango hiyo.

Rais Samia alisema taarifa hizio zitasaidia kujua wastani wa ongezeko la watu na hali ya uhamiaji mfano kutoka vijijini kuja mjini lakini hata waliotoka nje kuhamia na kuingia Tanzania.

"Sensa pia itatusaidia Serikali kufanya maamuzi kuhusu ugawaji wa rasilimali za Taifa na kupeleka huduma mbalimbali kwa wananchi ikiwemo afya, elimu, maji, umeme, ujenzi wa miundombinu kulingana na idadi ya watu na mahitaji ya maeneo hayo" alisema Rais Samia.

“Ili Sensa iweze kukidhi mahitaji ya kufanikisha malengo yote hayo ni lazima ishirikishe watu wote. Zoezi hili litakuwa ni kwa watu wote waliolala na kuamkia siku ya Sensa kwenye nchi ya Tanzania,” alisema Rais Samia.

Alisema licha ya uwepo wa tozo za makazi, Serikali haikuwa na idadi sahihi ya nyumba na makazi, hivyo zoezi hilo litatoa ubora kwa kujua anuani za makazi, idadi ya majumba na aina za nyumba zilizopo.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/78faf0bf8bfbbed01cba6bb8698c0fef.jpg

WASICHANA waliopata ujauzito katika umri mdogo ...

foto
Mwandishi: Na Rahimu Fadhili

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi